1 Chronicles 4:41 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Katika siku za mfalme Hezekia wa Yuda, watu hao waliotajwa majina yao walikwenda huko Gedori, wakaharibu hema za Wameuni waliokuwa wakiishi huko na kuwafukuza kabisa mpaka leo. Walifanya makao yao ya kudumu huko kwa sababu kulikuwa na malisho tele kwa ajili ya kondoo wao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu walioorodheshwa majina walikuja nchi hiyo wakati wa Hezekia mfalme wa Yuda. Wasimeoni wakawashambulia Wahamu katika makao yao pamoja na Wameuni ambao walikuwa huko, nao wakawaangamiza kabisa, kama ilivyo dhahiri hadi leo. Kisha wakaishi huko kwa sababu kulikuwa na malisho mazuri kwa mifugo yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na hao walioandikwa majina yao waliingia huko katika siku za Hezekia, mfalme wa Yuda, na kuzipiga hema zao, pamoja na hao Wameuni walioonekana huko, wakawaangamiza kabisa, hata siku hii ya leo, nao wakakaa huko badala yao; kwa sababu huko kulikuwa na malisho kwa kondoo zao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Katika siku za mfalme Hezekia wa Yuda, watu hao waliotajwa majina yao walikwenda huko Gedori, wakaharibu hema za Wameuni waliokuwa wakiishi huko na kuwafukuza kabisa mpaka leo. Walifanya makao yao ya kudumu huko kwa sababu kulikuwa na malisho tele kwa ajili ya kondoo wao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu walioorodheshwa majina walikuja katika nchi hiyo wakati wa Hezekia mfalme wa Yuda. Akawashambulia Wahamu katika makao yao pamoja na Wameuni ambao walikuwako huko nao wakawaangamiza kabisa, kama ilivyo dhahiri hadi leo. Kisha wakafanya makazi yao huko kwa sababu kulikuwa na malisho mazuri kwa ajili ya mifugo yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu walioorodheshwa majina walikuja katika nchi hiyo wakati wa Hezekia mfalme wa Yuda. Akawashambulia Wahamu katika makao yao pamoja na Wameuni ambao walikuwako huko nao wakawaangamiza kabisa, kama ilivyo dhahiri hadi leo. Kisha wakafanya makazi yao huko kwa sababu kulikuwa na malisho mazuri kwa ajili ya mifugo yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na hao walioandikwa majina yao waliingia huko katika siku za Hezekia, mfalme wa Yuda, na kuziharibu hema zao, pamoja na hao Wameuni waliokuwa wakiishi huko, wakawaangamiza kabisa, hata siku hii ya leo, nao wakakaa huko badala yao; kwa sababu huko kulikuwa na malisho kwa kondoo wao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Katika siku za mfalme Hezekia wa Yuda, watu hao waliotajwa majina yao walikwenda huko Gedori, wakaharibu hema za Wameuni waliokuwa wakiishi huko na kuwafukuza kabisa mpaka leo. Walifanya makao yao ya kudumu huko kwa sababu kulikuwa na malisho tele kwa ajili ya kondoo wao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wao walioandikwa majina hapo waliingia huko siku zake Hizikia, mfalme wa Yuda, wakayapiga mahema yao pamoja na Wameuni walioonekana huko, wakawatia mwiko wa kuwapo mpaka siku hii ya leo, wakakaa mahali pao, kwani malisho ya mbuzi na kondoo wao yalikuwapo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na hao walioandikwa majina yao waliingia huko katika siku za Hezekia, mfalme wa Yuda, na kuzipiga hema zao, pamoja na hao Wameuni walioonekana huko, wakawaangamiza kabisa, hata siku hii ya leo, nao wakakaa huko badala yao; kwa sababu huko kulikuwa na malisho kwa kondoo zao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika siku za utawala wa mufalme Hezekia wa Yuda, watu wale waliotajwa majina yao walikwenda kule Gedori, wakaharibu hema za Wameuni waliokuwa wakiishi kule na kuwafukuza kabisa mpaka leo. Wakafanya makao yao ya kudumu kule kwa sababu kulikuwa malisho tele kwa ajili ya kondoo wao.