1 Chronicles 5:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Pia, kwa maana mifugo yao iliongezeka kwa wingi sana, walisambaa upande wa mashariki hadi kwenye maingilio ya jangwa lililoenea hadi mto Eufrate.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa upande wa mashariki walienea hadi pembeni mwa jangwa linaloenea hadi kwenye Mto Frati, kwa sababu mifugo yao ilikuwa imeongezeka huko Gileadi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na upande wa mashariki akakaa hata kufika maingilio ya jangwa litokalo mto wa Frati; kwa sababu ng'ombe zao walikuwa wameongezeka sana katika nchi ya Gileadi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Pia, kwa maana mifugo yao iliongezeka kwa wingi sana, walisambaa upande wa mashariki hadi kwenye maingilio ya jangwa lililoenea hadi mto Eufrate.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa upande wa mashariki walienea hadi pembeni mwa jangwa linaloenea mpaka kwenye Mto Eufrati, kwa sababu mifugo yao ilikuwa imeongezeka huko Gileadi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa upande wa mashariki walienea hadi pembeni mwa jangwa linaloenea mpaka kwenye Mto Frati, kwa sababu mifugo yao ilikuwa imeongezeka huko Gileadi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na upande wa mashariki akakaa hadi mwanzoni mwa jangwa litokalo mto wa Frati; kwa sababu ng'ombe wao walikuwa wameongezeka sana katika nchi ya Gileadi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Pia, kwa maana mifugo yao iliongezeka kwa wingi sana, walisambaa upande wa mashariki hadi kwenye maingilio ya jangwa lililoenea hadi mto Eufrate.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Upande wa maawioni kwa jua alikaa mpaka kufika katika nyika iliyoko kwenye mto wa Furati, kwani makundi yalikuwa mengi katika nchi ya Gileadi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na upande wa mashariki akakaa hata kufika maingilio ya jangwa litokalo mto wa Frati; kwa sababu ng’ombe zao walikuwa wameongezeka sana katika nchi ya Gileadi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vilevile, kwa maana makundi yao ya nyama iliongezeka kwa wingi sana, walisambaa upande wa mashariki mpaka kwenye viingilio vya jangwa lililoenea mpaka kwenye muto Furati.