1 Chronicles 6:32 — Compare Translations

10 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walifanya kazi yao ya kuimba mbele ya hema takatifu la mkutano hadi wakati mfalme Solomoni alipojenga hekalu la Mwenyezi-Mungu huko Yerusalemu. Waliutekeleza wajibu wao barabara, kwa zamu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walihudumu kwa kuimba mbele ya Maskani, Hema la Kukutania, hadi hapo Mfalme Sulemani alipojenga Hekalu la Mwenyezi Mungu huko Yerusalemu. Walitimiza wajibu wao kulingana na taratibu walizokuwa wamewekewa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao wakafanya kazi yao ya kuimba mbele ya maskani ya hema ya kukutania, hata Sulemani alipokuwa amejenga ile nyumba ya Bwana huko Yerusalemu; pia wakaisimamia huduma yao sawasawa na zamu zao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walifanya kazi yao ya kuimba mbele ya hema takatifu la mkutano hadi wakati mfalme Solomoni alipojenga hekalu la Mwenyezi-Mungu huko Yerusalemu. Waliutekeleza wajibu wao barabara, kwa zamu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walihudumu kwa kuimba mbele ya Maskani, Hema la Kukutania, mpaka hapo Mfalme Solomoni alipojenga Hekalu la BWANA huko Yerusalemu. Walitimiza wajibu wao kulingana na taratibu walizokuwa wamewekewa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walihudumu kwa kuimba mbele ya Maskani, Hema la Kukutania, mpaka hapo Mfalme Sulemani alipojenga Hekalu la bwana huko Yerusalemu. Walitimiza wajibu wao kulingana na taratibu walizokuwa wamewekewa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao wakafanya kazi yao ya kuimba mbele ya maskani ya hema ya kukutania, hata Sulemani alipokuwa amejenga ile nyumba ya BWANA huko Yerusalemu; nao wakatoa huduma yao kwa kufuata zamu zao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walifanya kazi yao ya kuimba mbele ya hema takatifu la mkutano hadi wakati mfalme Solomoni alipojenga hekalu la Mwenyezi-Mungu huko Yerusalemu. Waliutekeleza wajibu wao barabara, kwa zamu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao walikuwa wakitumika mbele ya Kao la Hema la Mkutano kwa kuimba, mpaka Salomo alipoijenga Nyumba ya Bwana mle Yerusalemu, wakasimama katika kazi zao na kupokeana zamu kama desturi yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao wakafanya kazi yao ya kuimba mbele ya maskani ya hema ya kukutania, hata Sulemani alipokuwa amejenga ile nyumba ya BWANA huko Yerusalemu; pia wakaisimamia huduma yao sawasawa na zamu zao.