1 Chronicles 6:62 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ukoo wa Gershomu, kulingana na jamaa zake ulipewa miji kumi na mitatu katika kabila la Isakari, na katika kabila la Naftali na katika kabila la Manase katika Bashani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wazao wa Gershoni, kufuatana na koo zao, walipewa miji kumi na tatu kutoka kwa makabila ya Isakari, Asheri na Naftali, na kutoka sehemu ya kabila la Manase huko Bashani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na wana wa Gershoni walipewa kwa kura miji kumi na mitatu, sawasawa na jamaa zao, katika kabila ya Isakari, na katika kabila ya Asheri, na katika kabila ya Naftali, na katika kabila ya Manase waliokaa Bashani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ukoo wa Gershomu, kulingana na jamaa zake ulipewa miji kumi na mitatu katika kabila la Isakari, na katika kabila la Naftali na katika kabila la Manase katika Bashani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wazao wa Gershoni, ukoo kwa ukoo, walipewa miji kumi na mitatu kutoka kwa makabila ya Isakari, Asheri na Naftali kutoka sehemu ya kabila la Manase huko Bashani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wazao wa Gershoni, ukoo kwa ukoo, walipewa miji kumi na mitatu kutoka kwa makabila ya Isakari, Asheri na Naftali kutoka sehemu ya kabila la Manase huko Bashani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na wana wa Gershoni walipewa kwa kura miji kumi na mitatu, kulingana na jamaa zao, katika kabila la Isakari, na katika kabila la Asheri, na katika kabila la Naftali, na katika kabila la Manase waliokaa Bashani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ukoo wa Gershomu, kulingana na jamaa zake ulipewa miji kumi na mitatu katika kabila la Isakari, na katika kabila la Naftali na katika kabila la Manase katika Bashani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao wana wa Gersomu walipewa miji 13, iwe ya ukoo wao katika shina la Isakari na katika shina la Aseri na katika shina la Nafutali na katika shina la Manase huko Basani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na wana wa Gershoni walipewa kwa kura miji kumi na mitatu, sawasawa na jamaa zao, katika kabila ya Isakari, na katika kabila ya Asheri, na katika kabila ya Naftali, na katika kabila ya Manase waliokaa Bashani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Jamaa za Merari zilizobakia, zilipewa miji hii pamoja na mashamba yake ya malisho kandokando ya miji hiyo. Katika kabila la Zebuluni walipewa Rimono pamoja na mashamba yake ya malisho na Tabori pamoja na mashamba yake ya malisho.