1 Chronicles 6:71 — Compare Translations
10 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Jamaa za ukoo wa Gershomu walipewa miji ifuatayo pamoja na malisho yake: Katika nusu ya kabila la Manase walipewa: Golani katika Bashani pamoja na malisho yake, Ashtarothi pamoja na malisho yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wagershoni walipokea miji ifuatayo: Katika nusu ya kabila la Manase, walipokea Golani katika Bashani, na pia Ashtarothi, pamoja na maeneo ya malisho ya kila mji.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na wana wa Gershoni wakapewa, katika jamaa ya nusu-kabila ya Manase; Golani katika Bashani pamoja na viunga vyake, na Ashtarothi pamoja na viunga vyake;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Jamaa za ukoo wa Gershomu walipewa miji ifuatayo pamoja na malisho yake: katika nusu ya kabila la Manase walipewa: Golani katika Bashani pamoja na malisho yake, Ashtarothi pamoja na malisho yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wagerishoni walipokea miji ifuatayo pamoja na maeneo yake ya malisho: Katika nusu ya kabila la Manase: walipewa Golani katika Bashani na pia Ashtarothi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wagershoni walipokea miji ifuatayo pamoja na maeneo yake ya malisho: Katika nusu ya kabila la Manase: walipewa Golani katika Bashani na pia Ashtarothi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na wana wa Gershoni wakapewa, katika jamaa ya nusu kabila ya Manase; Golani katika Bashani pamoja na viunga vyake, na Ashtarothi pamoja na viunga vyake;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Jamaa za ukoo wa Gershomu walipewa miji ifuatayo pamoja na malisho yake: Katika nusu ya kabila la Manase walipewa: Golani katika Bashani pamoja na malisho yake, Ashtarothi pamoja na malisho yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wana wa Gersomu walipata katika ukoo wao wa nusu ya shina la Manase Golani ulioko Basani pamoja na malisho yake na Astaroti pamoja na malisho yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na wana wa Gershoni wakapewa, katika jamaa ya nusu-kabila ya Manase; Golani katika Bashani pamoja na viunga vyake, na Ashtarothi pamoja na viunga vyake;