1 Chronicles 7:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wote hawa walikuwa wakuu wa jamaa katika koo zao na askari mashujaa wa vita. Kutokana na wazawa wao, kulipatikana wanaume 178,200, wanajeshi hodari tayari kabisa kwa vita.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hawa wana wote wa Yediaeli walikuwa viongozi wa jamaa zao. Kulikuwa na wapiganaji elfu kumi na saba na mia mbili waliokuwa tayari kwa vita.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hao wote ndio wana wa Yediaeli, sawasawa na wakuu wa mbari za baba zao, watu hodari wa vita, kumi na saba elfu na mia mbili, wawezao kwenda vitani katika jeshi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wote hawa walikuwa wakuu wa jamaa katika koo zao na askari mashujaa wa vita. Kutokana na wazawa wao, kulipatikana wanaume 178,200, wanajeshi hodari tayari kabisa kwa vita.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hawa wana wote wa Yadiaeli walikuwa viongozi wa jamaa zao. Kulikuwako wanaume wapiganaji 17,200 waliokuwa tayari kwenda vitani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hawa wana wote wa Yediaeli walikuwa viongozi wa jamaa zao. Kulikuwako wanaume wapiganaji 17,200 waliokuwa tayari kwenda vitani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hao wote ndio wana wa Yediaeli, kulingana na wakuu wa koo za baba zao, watu hodari wa vita, elfu kumi na saba na mia mbili, wawezao kwenda vitani katika jeshi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wote hawa walikuwa wakuu wa jamaa katika koo zao na askari mashujaa wa vita. Kutokana na wazawa wao, kulipatikana wanaume 178,200, wanajeshi hodari tayari kabisa kwa vita.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hawa wote walikuwa wana wa Yediaeli, nao walikuwa vichwa vya milango ya baba zao na mafundi wa vita wenye nguvu nyingi, watu 17200 walioweza kutoka kwenda vitani kupigana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hao wote ndio wana wa Yediaeli, sawasawa na wakuu wa mbari za baba zao, watu hodari wa vita, kumi na saba elfu na mia mbili, wawezao kwenda vitani katika jeshi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wote hawa walikuwa wakubwa wa jamaa katika ukoo zao na waaskari mashujaa wa vita. Kutokana na wazao wao, kulipatikana wanaume elfu kumi na saba na mia mbili, waaskari hodari tayari kabisa kwa vita.