1 Chronicles 7:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Makiri aliwazaa Hupimu na Shupimu. Jina la dada yake lilikuwa Maaka. Mwana wa pili wa Makiri alikuwa Selofehadi. Selofehadi alikuwa na mabinti peke yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Makiri akatwaa mke kutoka miongoni mwa Wahupimu na Washupimu. Jina la dada yake Makiri aliitwa Maaka. Mwana mwingine wa Makiri aliitwa Selofehadi, aliyekuwa na watoto wa kike tu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
naye Makiri akatwaa mke kwa Hupimu na Shupimu, ambao umbu lao aliitwa Maaka; na wa pili akaitwa jina lake Selofehadi; na Selofehadi alikuwa na binti.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Makiri aliwazaa Hupimu na Shupimu. Jina la dada yake lilikuwa Maaka. Mwana wa pili wa Makiri alikuwa Selofehadi. Selofehadi alikuwa na mabinti peke yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Makiri akatwaa mke kutoka miongoni mwa Wahupimu na Washupimu. Jina la dada yake aliitwa Maaka. Mwana wa pili wa Makiri aliitwa Selofehadi, ambaye alikuwa na wasichana tu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Makiri akatwaa mke kutoka miongoni mwa Wahupimu na Washupimu. Jina la dada yake aliitwa Maaka. Mwana wa pili wa Makiri aliitwa Selofehadi, ambaye alikuwa na wasichana tu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
naye Makiri akatwaa mke kwa Hupimu na Shupimu, ambao dada yao aliitwa Maaka; na wa pili akaitwa jina lake Selofehadi; na Selofehadi alikuwa na binti.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Makiri aliwazaa Hupimu na Shupimu. Jina la dada yake lilikuwa Maaka. Mwana wa pili wa Makiri alikuwa Selofehadi. Selofehadi alikuwa na mabinti peke yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Makiri akawaoza Hupimu na Supimu, nalo jina la umbu lake ni Maka, nalo jina la mwanawe wa pili ni Selofuhadi, naye Selofuhadi alikuwa na wana wa kike tu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
naye Makiri akatwaa mke kwa Hupimu na Shupimu, ambao umbu lao aliitwa Maaka; na wa pili akaitwa jina lake Selofehadi; na Selofehadi alikuwa na binti.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Makiri alizaa Hupimu na Supimu. Jina la dada yake lilikuwa Maka. Mwana wa pili wa Makiri aliitwa Zolofehadi. Zolofehadi alikuwa na wabinti peke yake.