1 Chronicles 7:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wana wa Tola walikuwa: Uzi, Refaya, Yerieli, Yamai, Ibsamu na Shemueli. Hao walikuwa wakuu wa jamaa za koo za Tola na watu mashujaa sana wa vita nyakati zao. Idadi ya wazawa wao siku za mfalme Daudi ilikuwa 22,600.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wana wa Tola walikuwa: Uzi, Refaya, Yerieli, Yahmai, Ibsamu na Samweli waliokuwa viongozi wa jamaa zao. Wakati wa utawala wa Mfalme Daudi, wazao wa Tola walioorodheshwa kama wapiganaji katika ukoo wao walikuwa watu elfu ishirini na mbili na mia sita.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na wana wa Tola; Uzi, na Refaya, na Yerieli, na Yamai, na Ibsamu, na Shemueli, wakuu wa mbari za baba zao, yaani, wa Tola; watu hodari wa vita katika vizazi vyao; hesabu yao katika siku za Daudi ilikuwa watu ishirini na mbili elfu na mia sita.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wana wa Tola walikuwa: Uzi, Refaya, Yerieli, Yamai, Ibsamu na Shemueli. Hao walikuwa wakuu wa jamaa za koo za Tola na watu mashujaa sana wa vita nyakati zao. Idadi ya wazawa wao siku za mfalme Daudi ilikuwa 22,600.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wana wa Tola walikuwa: Uzi, Refaia, Yerieli, Yahmai, Ibsamu na Shemueli waliokuwa viongozi wa jamaa zao. Wakati wa utawala wa Mfalme Daudi, wazao wa Tola walioorodheshwa kama wapiganaji katika ukoo wao walikuwa watu 22,600.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wana wa Tola walikuwa: Uzi, Refaya, Yerieli, Yahmai, Ibsamu na Shemueli waliokuwa viongozi wa jamaa zao. Wakati wa utawala wa Mfalme Daudi, wazao wa Tola walioorodheshwa kama wapiganaji katika ukoo wao walikuwa watu 22,600.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na wana wa Tola; Uzi, na Refaya, na Yerieli, na Yamai, na Ibsamu, na Shemueli, wakuu wa koo za baba zao, yaani, wa Tola; watu hodari wa vita katika vizazi vyao; hesabu yao katika siku za Daudi ilikuwa watu elfu ishirini na mbili na mia sita.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wana wa Tola walikuwa: Uzi, Refaya, Yerieli, Yamai, Ibsamu na Shemueli. Hao walikuwa wakuu wa jamaa za koo za Tola na watu mashujaa sana wa vita nyakati zao. Idadi ya wazawa wao siku za mfalme Daudi ilikuwa 22,600.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao wana wa Tola: Uzi na Refaya na Yerieli na Yamai na Ibusamu na Samweli, hawa walikuwa vichwa vyao vya milango ya baba zao; wao wa Tola walikuwa mafundi wa vita wenye nguvu katika vizazi vyao, hesabu yao katika siku za Dawidi ilikuwa watu 22600.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na wana wa Tola; Uzi, na Refaya, na Yerieli, na Yamai, na Ibsamu, na Shemueli, wakuu wa mbari za baba zao, yaani, wa Tola; watu hodari wa vita katika vizazi vyao; hesabu yao katika siku za Daudi ilikuwa watu ishirini na mbili elfu na mia sita.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wana wa Tola walikuwa: Usi, Refaya, Yerieli, Yamai, Ibusamu na Semweli. Hao walikuwa wakubwa wa jamaa za ukoo za Tola na watu mashujaa sana wa vita nyakati zao. Hesabu ya wazao wao siku za utawala wa mufalme Daudi ilikuwa elfu makumi mbili na mbili na mia sita.