1 Chronicles 7:40 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hao wote walikuwa wazawa wa Asheri na walikuwa wakuu wa jamaa zao, watu wateule na hodari wa vita. Idadi ya wale walioandikishwa kwa kufuata koo katika jeshi ilikuwa 26,000.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hawa wote ndio walikuwa wazao wa Asheri, viongozi wa jamaa zao, watu bora, mashujaa hodari na viongozi maarufu. Idadi ya watu waliokuwa wamejiandaa kwa vita, kama walivyoorodheshwa katika ukoo wao, walikuwa elfu ishirini na sita.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hao wote ndio wana wa Asheri, wakuu wa mbari za baba zao, watu wateule, hodari wa vita, wakuu wa mashehe. Na hesabu yao waliojumlishwa kwa vizazi vyao kwenda vitani walikuwa watu ishirini na sita elfu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hao wote walikuwa wazawa wa Asheri na walikuwa wakuu wa jamaa zao, watu wateule na hodari wa vita. Idadi ya wale walioandikishwa kwa kufuata koo katika jeshi ilikuwa 26,000.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hawa wote ndio waliokuwa wazao wa Asheri, viongozi wa jamaa zao, watu bora, mashujaa walio hodari na viongozi maarufu. Idadi ya watu waliokuwa tayari kwa vita, kama ilivyoorodheshwa katika ukoo wao, walikuwa 26,000.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hawa wote ndio waliokuwa wazao wa Asheri, viongozi wa jamaa zao, watu bora, mashujaa walio hodari na viongozi maarufu. Idadi ya watu waliokuwa tayari kwa vita, kama ilivyoorodheshwa katika ukoo wao, walikuwa 26,000.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hao wote ndio wana wa Asheri, wakuu wa koo za baba zao, watu wateule, hodari wa vita, viongozi wa wakuu. Na hesabu yao waliojumlishwa kwa vizazi vyao kwenda vitani walikuwa watu elfu ishirini na sita.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hao wote walikuwa wazawa wa Asheri na walikuwa wakuu wa jamaa zao, watu wateule na hodari wa vita. Idadi ya wale walioandikishwa kwa kufuata koo katika jeshi ilikuwa 26,000.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hawa wote walikuwa wana wa Aseri, vichwa vya milango ya baba zao, mafundi wa vita wenye nguvu nyingi waliochaguliwa, wawe vichwa vya wakuu; wao walioandikwa katika kitabu cha udugu kuwa katika vikosi vya wapiga vita hesabu yao ilikuwa watu 26000.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hao wote ndio wana wa Asheri, wakuu wa mbari za baba zao, watu wateule, hodari wa vita, wakuu wa mashehe. Na hesabu yao waliojumlishwa kwa vizazi vyao kwenda vitani walikuwa watu ishirini na sita elfu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hao wote walikuwa wazao wa Aseri na walikuwa wakubwa wa jamaa zao, watu wafundi na hodari wa vita. Hesabu ya wale walioandikwa kwa kufuata ukoo katika kundi la waaskari ilikuwa elfu makumi mbili na sita.