1 Chronicles 9:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hadi kufikia wakati huo, walinzi kutoka katika koo zao ndio waliolinda Lango la mfalme la upande wa mashariki. Hapo awali, walikuwa walinzi wa maingilio ya makambi ya Walawi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walikuwa wamewekwa katika lango la mfalme lililokuwa upande wa mashariki, hadi wakati huu. Hawa walikuwa mabawabu kutoka kambi ya Walawi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ambao tangu hapo walikuwa wakingojea penye lango la mfalme upande wa mashariki; hao ndio waliokuwa wangojezi wa rago la wana wa Lawi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hadi kufikia wakati huo, walinzi kutoka katika koo zao ndio waliolinda Lango la mfalme la upande wa mashariki. Hapo awali, walikuwa walinzi wa maingilio ya makambi ya Walawi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walikuwa wamewekwa katika lango la mfalme lililokuwa upande wa mashariki, mpaka wakati huu. Hawa walikuwa mabawabu wa kutoka kwenye kambi ya Walawi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walikuwa wamewekwa katika lango la mfalme lililokuwa upande wa mashariki, mpaka wakati huu. Hawa walikuwa mabawabu wa kutoka kwenye kambi ya Walawi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ambao tangu hapo walikuwa wakilinda penye lango la mfalme upande wa mashariki; hao ndio waliokuwa walinzi wa kambi ya wana wa Lawi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hadi kufikia wakati huo, walinzi kutoka katika koo zao ndio waliolinda Lango la mfalme la upande wa mashariki. Hapo awali, walikuwa walinzi wa maingilio ya makambi ya Walawi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
naye anashika mpaka leo zamu ya lango la mfalme lililoko upande wa maawioni kwa jua. Hawa ndio walinda malango wa makambi ya wana wa Lawi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ambao tangu hapo walikuwa wakingojea penye lango la mfalme upande wa mashariki; hao ndio waliokuwa wangojezi wa rago la wana wa Lawi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hata kufikia wakati ule, walinzi kutoka katika ukoo zao ndio waliolinda mulango wa mufalme wa upande wa mashariki. Zamani, walikuwa walinzi wa viingilio vya makambi ya Walawi.