1 Chronicles 9:19 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Shalumu, mwana wa Kore, mwana wa Ebiasafu, pamoja na ndugu zake wa ukoo wa Kora, walikuwa na wajibu wa kuyatunza maingilio ya hema la mkutano, kama vile walivyokuwa babu zake wakati wa ulinzi wa kambi ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Shalumu mwana wa Kore, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora, pamoja na mabawabu wenzake kutoka jamaa yake ya Kora waliwajibika kulinda malango ya Hema, kama baba zao walivyokuwa wamewajibika kulinda ingilio la Maskani ya Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Shalumu, mwana wa Kore, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora; pamoja na nduguze wa mbari ya babaye, Wakora; walikuwa wakiisimamia kazi hiyo ya huduma, wenye ungojezi wa malango ya maskani; na baba zao walikuwa wamesimamia matuo ya Bwana, wakiyalinda maingilio;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Shalumu, mwana wa Kore, mwana wa Ebiasafu, pamoja na ndugu zake wa ukoo wa Kora, walikuwa na wajibu wa kuyatunza maingilio ya hema la mkutano, kama vile walivyokuwa babu zake wakati wa ulinzi wa kambi ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Shalumu mwana wa Kore, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora, pamoja na mabawabu wenzake kutoka jamaa yake (ya Wakora) waliwajibika kulinda sakafu ya kupuria nafaka ya Hema, kama vile baba zao walivyokuwa wamewajibika kulinda ingilio la Maskani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Shalumu mwana wa Kore, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora, pamoja na mabawabu wenzake kutoka jamaa yake ya Kora waliwajibika kulinda malango ya Hema, kama vile baba zao walivyokuwa wamewajibika kulinda ingilio la Maskani ya bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Shalumu, mwana wa Kore, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora; pamoja na nduguze wa ukoo wa babaye, Wakora; walikuwa wakiisimamia kazi hiyo ya huduma, wenye ulinzi wa malango ya maskani; na kama vile baba zao walivyokuwa wamesimamia kambi ya BWANA, wakiyalinda maingilio;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Shalumu, mwana wa Kore, mwana wa Ebiasafu, pamoja na ndugu zake wa ukoo wa Kora, walikuwa na wajibu wa kuyatunza maingilio ya hema la mkutano, kama vile walivyokuwa babu zake wakati wa ulinzi wa kambi ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Salumu, mwana wa Kore, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora, na ndugu zake wa mlango wa baba yake wao Wakora, walikuwa wenye kazi za utumishi wa kuwa wangoja vizingiti vya hilo Hema, nao baba zao walikuwa wakingoja pa kuyaingilia makambi ya Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Shalumu, mwana wa Kore, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora; pamoja na nduguze wa mbari ya babaye, Wakora; walikuwa wakiisimamia kazi hiyo ya huduma, wenye ungojezi wa malango ya maskani; na baba zao walikuwa wamesimamia matuo ya BWANA, wakiyalinda maingilio;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Salumu mwana wa Kore mwana wa Ebiasafu, pamoja na wandugu zake wa ukoo wa Kora, walikuwa na kazi ya kutunza viingilio vya hema la mukutano, kama vile babu zake walivyokuwa wakati wa ulinzi wa kambi ya Yawe.