1 Chronicles 9:22 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Jumla, watu 212 walichaguliwa kuwa walinzi wa maingilio ya hekalu. Waliandikishwa kulingana na vijiji walimoishi. Mfalme Daudi na Samueli mwonaji ndio waliowathibitisha katika wadhifa huu muhimu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Jumla ya waliochaguliwa kuwa mabawabu katika sakafu za kupuria nafaka walikuwa watu mia mbili na kumi na wawili (212). Waliandikishwa kwa koo zao kwenye vijiji vyao. Mabawabu hawa waliwekwa katika nafasi zao za kuaminiwa na Daudi, pamoja na Samweli aliyekuwa mwonaji.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hao wote waliochaguliwa kuwa wangojezi wa malango walikuwa watu mia mbili na kumi na wawili. Nao wakahesabiwa kwa nasaba katika vijiji vyao, ambao Daudi na Samweli, huyo mwonaji, walikuwa wamewaweka katika kazi yao waliyoamaniwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Jumla, watu 212 walichaguliwa kuwa walinzi wa maingilio ya hekalu. Waliandikishwa kulingana na vijiji walimoishi. Mfalme Daudi na Samueli mwonaji ndio waliowathibitisha katika wadhifa huu muhimu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Jumla ya waliochaguliwa kuwa mabawabu katika sakafu za kupuria nafaka walikuwa watu 212. Waliandikishwa kwa koo zao kwenye vijiji vyao. Mabawabu hawa waliwekwa katika nafasi zao walizokabidhiwa na Mfalme Daudi pamoja na mwonaji Samweli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Jumla ya waliochaguliwa kuwa mabawabu katika sakafu za kupuria nafaka walikuwa watu 212. Waliandikishwa kwa koo zao kwenye vijiji vyao. Mabawabu hawa waliwekwa katika nafasi zao za kuaminiwa na Daudi pamoja na mwonaji Samweli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hao wote waliochaguliwa kuwa walinzi wa malango walikuwa watu mia mbili na kumi na wawili. Nao wakahesabiwa kwa nasaba katika vijiji vyao, ambao Daudi na Samweli, huyo mwonaji, walikuwa wamewaweka katika kazi yao waliyotegemewa kwayo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Jumla, watu 212 walichaguliwa kuwa walinzi wa maingilio ya hekalu. Waliandikishwa kulingana na vijiji walimoishi. Mfalme Daudi na Samueli mwonaji ndio waliowathibitisha katika wadhifa huu muhimu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wao wote waliochaguliwa, wawe walinda vizingiti, walikuwa watu 212; nao walikuwa wameandikwa katika kitabu cha udugu katika vijiji vyao; wao ndio, Dawidi na mtazamaji Samweli waliowaweka kwa kuwategemea.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hao wote waliochaguliwa kuwa wangojezi wa malango walikuwa watu mia mbili na kumi na wawili. Nao wakahesabiwa kwa nasaba katika vijiji vyao, ambao Daudi na Samweli, huyo mwonaji, walikuwa wamewaweka katika kazi yao waliyoamaniwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa jumla, watu mia mbili na kumi na wawili walichaguliwa kuwa walinzi wa viingilio vya hekalu. Waliandikwa kulingana na vijiji walimoishi. Mufalme Daudi na nabii Samweli ndio waliowaweka kwa kazi zao kwa sababu ya uaminifu wao.