1 Chronicles 9:26 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
kwa maana wale walinzi wakuu wanne, ambao walikuwa Walawi, walikuwa na wajibu wa kusimamia vyumba na hazina ya nyumba ya Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini mabawabu wanne wakuu, waliokuwa Walawi, walikabidhiwa wajibu wa kusimamia vyumba na hazina katika nyumba ya Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kwa maana wale wangojezi wanne, waliokuwa wakuu, nao ni Walawi, walikuwa na kazi ya kuamaniwa, tena walikuwa juu ya vyumba na juu ya hazina katika nyumba ya Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
kwa maana wale walinzi wakuu wanne, ambao walikuwa Walawi, walikuwa na wajibu wa kusimamia vyumba na hazina ya nyumba ya Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini mabawabu wanne wakuu, ambao walikuwa Walawi, walikabidhiwa wajibu kwa ajili ya vyumba na hazina katika nyumba ya Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini mabawabu wanne wakuu, waliokuwa Walawi, walikabidhiwa wajibu kwa ajili ya vyumba na hazina katika nyumba ya Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kwa maana wale walinzi wanne, waliokuwa wakuu, nao ni Walawi, waliwajibika kuvilinda vyumba na hazina ya nyumba ya Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
kwa maana wale walinzi wakuu wanne, ambao walikuwa Walawi, walikuwa na wajibu wa kusimamia vyumba na hazina ya nyumba ya Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao hawa walinda malango walikuwa na wakuu wanne, hao walikaa hapohapo, kwani walitegemewa hivi. Hizi zilikuwa kazi zao Walawi, tena waliwekwa kuviangalia vyumba na vilimbiko vya Nyumbani mwa Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kwa maana wale wangojezi wanne, waliokuwa wakuu, nao ni Walawi, walikuwa na kazi ya kuamaniwa, tena walikuwa juu ya vyumba na juu ya hazina katika nyumba ya Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
kwa maana wale walinzi wakubwa wane, ambao walikuwa Walawi, walikuwa na kazi ya kusimamia vyumba na hazina ya nyumba ya Mungu.