1 Chronicles 9:33 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Jamaa nyingine za Walawi zilisimamia huduma ya nyimbo hekaluni. Waliishi katika baadhi ya majengo ya nyumba ya Mungu na hawakuhitajika kufanya kazi nyingine yoyote kwa maana walikuwa kazini usiku na mchana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wale waliokuwa waimbaji, viongozi wa jamaa za Walawi, waliishi katika vyumba vya Hekalu, nao hawakufanya shughuli nyingine yoyote kwa sababu iliwapasa kuwajibika kwa kazi hiyo usiku na mchana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena hawa ndio waimbaji, wakuu wa mbari za baba zao katika Walawi, ambao walikaa vyumbani, kisha walikuwa hawana kazi nyingine; kwa kuwa walitumika katika kazi yao mchana na usiku.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Jamaa nyingine za Walawi zilisimamia huduma ya nyimbo hekaluni. Waliishi katika baadhi ya majengo ya nyumba ya Mungu na hawakuhitajika kufanya kazi nyingine yoyote kwa maana walikuwa kazini usiku na mchana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wale waliokuwa waimbaji, viongozi wa jamaa za Walawi, waliishi katika vyumba vya Hekalu, nao hawakufanya shughuli nyingine yo yote kwa sababu iliwapasa kuwajibika kwa kazi hiyo mchana na usiku.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wale waliokuwa waimbaji, viongozi wa jamaa za Walawi, waliishi katika vyumba vya Hekalu, nao hawakufanya shughuli nyingine yoyote kwa sababu iliwapasa kuwajibika kwa kazi hiyo usiku na mchana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena hawa ndio waimbaji, wakuu wa koo za baba zao katika Walawi, ambao walikaa vyumbani, kisha walikuwa hawana kazi nyingine; kwa kuwa walifanya kazi yao mchana na usiku.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Jamaa nyingine za Walawi zilisimamia huduma ya nyimbo hekaluni. Waliishi katika baadhi ya majengo ya nyumba ya Mungu na hawakuhitajika kufanya kazi nyingine yoyote kwa maana walikuwa kazini usiku na mchana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao hao ndio waimbaji waliokuwa vichwa vya milango ya baba zao ya Walawi, ndio waliokaa katika vile vyumba, wasiokuwa na kazi nyingine, kwani kazi yao yenyewe iliwataka mchana na usiku.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena hawa ndio waimbaji, wakuu wa mbari za baba zao katika Walawi, ambao walikaa vyumbani, kisha walikuwa hawana kazi nyingine; kwa kuwa walitumika katika kazi yao mchana na usiku.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Jamaa zingine za Walawi zilisimamia kazi ya nyimbo katika hekalu. Waliishi katika vyumba vimoja vya majengo ya nyumba ya Mungu na hawakuhitajika kufanya kazi ingine yoyote kwa maana walikuwa wakitumika usiku na muchana.