1 Corinthians 1:11 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndugu zangu, habari nilizopata kutoka kwa watu kadhaa wa jamaa ya Kloe, zaonesha wazi kwamba kuna kutoelewana kati yenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndugu zangu, nimepata habari kutoka kwa baadhi ya watu wa nyumbani mwa Kloe kwamba kuna magomvi kati yenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana, ndugu zangu, nimearifiwa habari zenu na wale walio wa nyumbani mwa Kloe, ya kwamba iko fitina kwenu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kaka na dada zangu, baadhi ya jamaa wa Kloe wamenitaarifu kuwa kuna mabishano miongoni mwenu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ndugu zangu, habari nilizopata kutoka kwa watu kadhaa wa jamaa ya Kloe, zaonyesha wazi kwamba kuna kutoelewana kati yenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndugu zangu, habari nilizopata kutoka kwa watu kadhaa wa jamaa ya Kloe, zaonesha wazi kwamba kuna kutoelewana kati yenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana ndugu zangu, nimepata habari kutoka kwa baadhi ya watu wa nyumbani mwa Kloe kwamba kuna magomvi katikati yenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndugu zangu, nimepata habari kutoka kwa baadhi ya watu wa nyumbani mwa Kloe kwamba kuna magomvi katikati yenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana, ndugu zangu, nimearifiwa habari zenu na wale walio wa nyumbani mwa Kloe, ya kwamba uko ugomvi kwenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndugu zangu, habari nilizopata kutoka kwa watu kadhaa wa jamaa ya Kloe, zaonesha wazi kwamba kuna kutoelewana kati yenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani ndugu zangu, nimeambiwa mambo yenu na wale wa Kloe, ya kuwa kwenu yako magomvi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana, ndugu zangu, nimearifiwa habari zenu na wale walio wa nyumbani mwa Kloe, ya kwamba iko fitina kwenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana, wandugu zangu, nimepata habari zenu kwa njia ya jamaa ya Kloe kwamba kuko ugomvi katikati yenu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana nimearifiwa khabari zenu, ndugu, na wale walio wa nyumba ya Kloe, ya kwamba iko fitina kwenu.