1 Corinthians 1:16 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Samahani, nilibatiza pia jamaa ya Stefana; lakini zaidi ya hawa, sidhani kama nilimbatiza mtu mwingine yeyote).
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
(Naam, niliwabatiza pia watu wa nyumbani mwa Stefana; lakini zaidi ya hao sijui kama nilimbatiza mtu mwingine yeyote.)
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena naliwabatiza watu wa nyumbani mwa Stefana; zaidi ya hao, sijui kama nalimbatiza mtu ye yote mwingine.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
(Niliwabatiza pia watu wote wa nyumbani mwa Stefana, lakini sikumbuki kuwa niliwabatiza watu wengine)
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
(Samahani, nilibatiza pia jamaa ya Stefana; lakini zaidi ya hawa, sidhani kama nilimbatiza mtu mwingine yeyote.)
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Samahani, nilibatiza pia jamaa ya Stefana; lakini zaidi ya hawa, sidhani kama nilimbatiza mtu mwingine yeyote).
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
(Naam, niliwabatiza pia watu wa nyumbani mwa Stefana. Lakini zaidi ya hao sijui kama nilimbatiza mtu mwingine ye yote.)
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
(Naam, niliwabatiza pia watu wa nyumbani mwa Stefana. Lakini zaidi ya hao sijui kama nilimbatiza mtu mwingine yeyote.)
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena niliwabatiza watu wa nyumbani mwa Stefana; zaidi ya hao, sijui kama nilimbatiza mtu yeyote mwingine.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Samahani, nilibatiza pia jamaa ya Stefana; lakini zaidi ya hawa, sidhani kama nilimbatiza mtu mwingine yeyote).
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kweli naliwabatiza nao wa nyumbani mwa Stefana. Tena sijui, kama yuko mwingine, niliyembatiza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena naliwabatiza watu wa nyumbani mwa Stefana; zaidi ya hao, sijui kama nalimbatiza mtu ye yote mwingine.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ni kweli, nilibatiza vilevile jamaa ya Stefano, zaidi ya wale sikumbuki kama nilibatiza mutu mwingine.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Tena nalibatiza watu wa nyumba ya Stefano; zaidi ya hao, sijui kama nalimbatiza mtu mwingine.