1 Corinthians 1:17 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kristo hakunituma kubatiza, bali kuhubiri Habari Njema; tena, niihubiri bila kutegemea maarifa ya hotuba za watu, kusudi nguvu ya kifo cha Kristo msalabani isibatilishwe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana Al-Masihi hakunituma ili kubatiza bali kuhubiri Injili; sio kwa maneno ya hekima ya kibinadamu, ili msalaba wa Al-Masihi usije ukakosa nguvu yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana Kristo hakunituma ili nibatize, bali niihubiri Habari Njema; wala si kwa hekima ya maneno, msalaba wa Kristo usije ukabatilika.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kristo hakunipa kazi ya kubatiza watu. Alinipa kazi ya kuhubiri Habari Njema pasipo kutumia hekima ya maneno, inayoweza kubatilisha nguvu iliyo katika msalaba wa Kristo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kristo hakunituma kubatiza, bali kuhubiri Habari Njema; tena, niihubiri bila kutegemea maarifa ya hotuba za watu kusudi nguvu ya kifo cha Kristo msalabani isibatilishwe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kristo hakunituma kubatiza, bali kuhubiri Habari Njema; tena, niihubiri bila kutegemea maarifa ya hotuba za watu, kusudi nguvu ya kifo cha Kristo msalabani isibatilishwe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana Kristo hakunituma ili kubatiza bali kuhubiri Injili na nifanye hivyo si kwa kutumia maneno ya hekima ya kibinadamu ya kushawishi, ili msalaba wa Kristo usije ukakosa nguvu yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana Al-Masihi hakunituma ili kubatiza bali kuhubiri Injili; sio kwa maneno ya hekima ya kibinadamu, ili msalaba wa Al-Masihi usije ukakosa nguvu yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana Kristo hakunituma ili nibatize, bali niihubiri Habari Njema; wala si kwa hekima ya maneno, msalaba wa Kristo usije ukabatilika.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kristo hakunituma kubatiza, bali kuhubiri Habari Njema; tena, niihubiri bila kutegemea maarifa ya hotuba za watu, kusudi nguvu ya kifo cha Kristo msalabani isibatilishwe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani Kristo hakunituma kubatiza, ila amenituma kuipiga hiyo mbiu njema, lakini si kwa maneno ya ujuzi wa kimtu, msalaba wake Kristo usitenguliwe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana Kristo hakunituma ili nibatize, bali niihubiri Habari Njema; wala si kwa hekima ya maneno, msalaba wa Kristo usije ukabatilika.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kristo hakunituma kwa kubatiza, lakini amenituma kwa kutangaza Habari Njema. Amenituma kuitangaza bila kutumia hekima ya usemi, kusudi uwezo unaotokana na kufa kwa Kristo juu ya musalaba usihesabiwe kuwa bure.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana Kristo hakunituma illi nibatize, bali niikhubiri Injili; wala si kwa hekima ya maneno, msalaba wa Kristo nsije nkabatilika.