1 Corinthians 1:25 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana kinachoonekana kuwa ni upumbavu wa Mungu, kina busara kuliko hekima ya binadamu; na kinachoonekana kuwa ni udhaifu wa Mungu, kina nguvu kuliko nguvu za binadamu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya hekima ya wanadamu, nao udhaifu wa Mungu una nguvu kuliko nguvu ya wanadamu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Maana upumbavu wa Mungu ni hekima zaidi ya hekima ya kibinadamu, na udhaifu wa Mungu ni nguvu zaidi ya nguvu ya kibinadamu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana kinachoonekana kuwa ni upumbavu wa Mungu, kina busara zaidi kuliko hekima ya binadamu; na kinachoonekana kuwa ni udhaifu wa Mungu, kina nguvu zaidi kuliko nguvu za binadamu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana kinachoonekana kuwa ni upumbavu wa Mungu, kina busara kuliko hekima ya binadamu; na kinachoonekana kuwa ni udhaifu wa Mungu, kina nguvu kuliko nguvu za binadamu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana upumbavu wa Mungu una hekima zaidi kuliko hekima ya wanadamu, nao udhaifu wa Mungu una nguvu kuliko nguvu ya wanadamu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana upumbavu wa Mwenyezi Mungu una hekima zaidi kuliko hekima ya wanadamu, nao udhaifu wa Mungu una nguvu kuliko nguvu ya wanadamu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana kinachoonekana kuwa ni upumbavu wa Mungu, kina busara kuliko hekima ya binadamu; na kinachoonekana kuwa ni udhaifu wa Mungu, kina nguvu kuliko nguvu za binadamu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani yaliyo mapumbavu ya Mungu ndiyo yenye werevu wa kweli kuupita wa watu, nayo yaliyo manyonge ya Mungu ndiyo yenye nguvu kuzipita za watu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana mambo wanayomuhesabilia Mungu kuwa ya upumbafu, yanapita hekima ya watu; nayo mambo yale wanayomuhesabilia kuwa ya uzaifu yanapita nguvu za watu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wana Adamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wana Adamu.