1 Corinthians 1:27 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndiyo kusema, Mungu aliyachagua yale ambayo ulimwengu huyaona ni upumbavu, ili awaaibishe wenye hekima; na aliyachagua yale ambayo ulimwengu huyaona ni dhaifu, ili awaaibishe wenye nguvu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Mungu alivichagua vitu vipumbavu vya ulimwengu ili awaaibishe wenye hekima; Mungu alivichagua vitu dhaifu vya ulimwengu ili awaaibishe wenye nguvu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini Mungu aliyachagua mambo ambayo wanadamu huyachukulia kuwa ya kipumbavu ili ayaaibishe yenye hekima. Aliyachagua mambo yanayoonekana kuwa manyonge ili ayaaibishe yenye nguvu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ndiyo kusema, Mungu aliyachagua yale ambayo ulimwengu huyaona ni upumbavu, ili awaaibishe wenye hekima; na aliyachagua yale ambayo ulimwengu huyaona ni dhaifu, ili awaaibishe wenye nguvu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndiyo kusema, Mungu aliyachagua yale ambayo ulimwengu huyaona ni upumbavu, ili awaaibishe wenye hekima; na aliyachagua yale ambayo ulimwengu huyaona ni dhaifu, ili awaaibishe wenye nguvu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Mungu alivichagua vitu vipumbavu vya ulimwengu ili aviaibishe vyenye hekima, Mungu alivichagua vitu dhaifu vya ulimwengu ili aviaibishe vyenye nguvu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Mwenyezi Mungu alivichagua vitu vipumbavu vya ulimwengu ili awaaibishe wenye hekima, Mungu alivichagua vitu dhaifu vya ulimwengu ili awaaibishe wenye nguvu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndiyo kusema, Mungu aliyachagua yale ambayo ulimwengu huyaona ni upumbavu, ili awaaibishe wenye hekima; na aliyachagua yale ambayo ulimwengu huyaona ni dhaifu, ili awaaibishe wenye nguvu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini walio wapumbavu wa ulimwengu huu ndio, Mungu aliowachagua, awatweze walio werevu wa kweli. Tena walio wanyonge wa ulimwengu huu ndio, Mungu aliowachagua, awatweze wenye nguvu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Mungu anachagua vitu ambavyo watu wanahesabu kuwa vya upumbafu kusudi apatishe wenye hekima haya, naye amechagua vitu wanavyohesabu kuwa vya uzaifu kusudi apatishe wenye nguvu haya.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
bali Mungu aliyachagua mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena alivichagua vitu dhaifu vya dunia illi wenye nguvu waaibishwe;