1 Corinthians 1:30 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mungu mwenyewe ndiye aliyewaunganisha nyinyi na Kristo Yesu. Mungu amemfanya Kristo awe hekima yetu; kwa njia yake sisi tunapatanishwa na Mungu, tunakuwa watu wake Mungu na kukombolewa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Al-Masihi Isa, aliyefanyika kwetu hekima inayotoka kwa Mungu, yaani haki yetu, na utakatifu na ukombozi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini Mungu ameyafungamanisha maisha yenu na Kristo Yesu. Yeye alifanywa kuwa hekima yetu kutoka kwa Mungu. Na kupitia kwake tumehesabiwa haki na Mungu na tumefanywa kuwa watakatifu. Kristo ndiye aliyetuokoa, akatufanya watakatifu na akatuweka huru mbali na dhambi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mungu mwenyewe ndiye aliyewaunganisha ninyi na Kristo Yesu. Mungu amemfanya Kristo awe hekima yetu; kwa njia yake sisi tunapatanishwa na Mungu, tunakuwa watu wake Mungu na kukombolewa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mungu mwenyewe ndiye aliyewaunganisha nyinyi na Kristo Yesu. Mungu amemfanya Kristo awe hekima yetu; kwa njia yake sisi tunapatanishwa na Mungu, tunakuwa watu wake Mungu na kukombolewa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mungu ndiye chanzo cha uzima wenu katika Kristo Yesu, aliyefanyika kwetu hekima itokayo kwa Mungu na haki na utakaso na ukombozi,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Al-Masihi Isa, aliyefanyika kwetu hekima itokayo kwa Mungu, yaani haki, na utakatifu na ukombozi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mungu mwenyewe ndiye aliyewaunganisha nyinyi na Kristo Yesu. Mungu amemfanya Kristo awe hekima yetu; kwa njia yake sisi tunapatanishwa na Mungu, tunakuwa watu wake Mungu na kukombolewa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwake yeye ndio, mlikotoka ninyi mliomo mwake Kristo Yesu. Huyu ndiye werevu wetu wa Kimungu ulio wa kweli, na wongufu na utakasi na ukombozi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Mungu amewaunganisha na Yesu Kristo, naye amemufanya Kristo kuwa hekima yetu. Kwa njia ya Kristo tunahesabiwa haki mbele ya Mungu, tumekuwa watu watakatifu wa Mungu, na kukombolewa toka zambi zetu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyekuwa kwenu hekima itokayo kwa Mungu na haki na utakatifu na ukombozi;