1 Corinthians 10:16 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tunapomshukuru Mungu kwa kikombe kile cha baraka, je, huwa hatushiriki damu ya Kristo? Na tunapoumega mkate, je, huwa hatushiriki mwili wa Kristo?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, kikombe cha baraka ambacho tunakibariki, si ushirika katika damu ya Al-Masihi? Mkate tunaoumega, si ushirika wa mwili wa Al-Masihi?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, je! Si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kikombe cha baraka tunachokitolea shukrani ni ushirika wa sadaka ya damu ya Kristo, sawa? Na mkate ule tunaomega, ni ushirika wa mwili wa Kristo, sawa?
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Tunapomshukuru Mungu kwa kikombe kile cha baraka, je, huwa hatushiriki damu ya Kristo? Na tunapoumega mkate, je, huwa hatushiriki mwili wa Kristo?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tunapomshukuru Mungu kwa kikombe kile cha baraka, je, huwa hatushiriki damu ya Kristo? Na tunapoumega mkate, je, huwa hatushiriki mwili wa Kristo?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, kikombe cha baraka ambacho tunakibariki, si ushirika katika damu ya Kristo? Mkate tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, kikombe cha baraka ambacho tunakibariki, si ushirika katika damu ya Al-Masihi? Mkate tuumegao, si ushirika wa mwili wa Al-Masihi?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, je! Si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tunapomshukuru Mungu kwa kikombe kile cha baraka, je, huwa hatushiriki damu ya Kristo? Na tunapoumega mkate, je, huwa hatushiriki mwili wa Kristo?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kinyweo chenye mbaraka, tukibarikicho, hakitupatii bia ya damu yake Kristo? Mkate, tuumegao, hautupatii bia ya mwili wake Kristo?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, je! Si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
tunapokunywa kikombe ambacho kwa ajili yake tunamutolea Mungu shukrani, basi kwa njia ya kikombe kile hatuungani na damu ya Kristo? Nasi tunapomega mukate na kuukula, kwa njia hiyo, mukate ule hautuungi na mwili wa Kristo?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, je! si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule timmegao, si ushirika wa mwili wti Kristo?