1 Corinthians 10:20 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hata kidogo! Ninachosema ni kwamba tambiko wanazotoa watu wasiomjua Mungu wanawatolea pepo, sio Mungu. Sipendi kamwe nyinyi muwe na ushirika na pepo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
La hasha! Lakini sadaka za watu wasiomjua Mungu hutolewa kwa mashetani, wala si kwa Mungu. Nami sitaki ninyi mwe na ushirika na mashetani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini ninasema kuwa chakula kinapotolewa sadaka kwa sanamu, ni sadaka kwa mashetani, siyo kwa Mungu. Nami sitaki ninyi muungane na hao wengine katika kuyaabudu mashetani.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hata kidogo! Ninachosema ni kwamba tambiko wanazotoa watu wasiomjua Mungu wanawatolea pepo, sio Mungu. Sipendi kamwe ninyi muwe na ushirika na pepo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hata kidogo! Ninachosema ni kwamba tambiko wanazotoa watu wasiomjua Mungu wanawatolea pepo, sio Mungu. Sipendi kamwe nyinyi muwe na ushirika na pepo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
La hasha! Lakini kafara za watu wasiomjua Mungu hutolewa kwa mashetani, wala si kwa Mungu. Nami sitaki ninyi mwe na ushirika na mashetani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
La hasha! Lakini kafara za watu wasiomjua Mwenyezi Mungu hutolewa kwa mashetani, wala si kwa Mungu. Nami sitaki ninyi mwe na ushirika na mashetani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hata kidogo! Ninachosema ni kwamba tambiko wanazotoa watu wasiomjua Mungu wanawatolea pepo, sio Mungu. Sipendi kamwe nyinyi muwe na ushirika na pepo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siyo, maana wamizimu waitambikia mizimu yao, hawamtambikii Mungu. Nami sitaki, ninyi mwe wenye bia na mizimu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hapana. Ninataka kusema kwamba vitu wapagani wanavyotambikia, wanavitolea pepo wala si Mungu. Nami sipendi mushirikiane na pepo hata mara moja.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo mataifi, wavitolea mashetani, wala si Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani.