1 Corinthians 10:27 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama mtu ambaye si mwaamini akiwaalikeni nanyi mkakubali kwenda, basi, kuleni vyote atakavyowaandalieni bila kuulizauliza kwa sababu ya dhamiri zenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ukikaribishwa chakula na mtu asiyeamini nawe ukikubali kwenda, kula kila kitu kitakachowekwa mbele yako bila kuuliza maswali kwa ajili ya dhamiri.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mtu asiyeamini akiwaalika, nanyi mnataka kwenda, kuleni kila kitu kiwekwacho mbele yenu bila kuuliza-uliza, kwa ajili ya dhamiri.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Asiye mwamini anaweza kuwaalika kula chakula. Ikiwa mtakwenda, basi mle chochote kitakachowekwa mbele yenu. Msiulize ulize maswali.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kama mtu ambaye si muumini akiwaalikeni nanyi mkakubali kwenda, basi, kuleni vyote atakavyowaandalieni bila kuulizauliza kwa sababu ya dhamiri zenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama mtu ambaye si mwaamini akiwaalikeni nanyi mkakubali kwenda, basi, kuleni vyote atakavyowaandalieni bila kuulizauliza kwa sababu ya dhamiri zenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama ukikaribishwa chakula na mtu asiyeamini nawe ukikubali kwenda, kula kila kitu kitakachowekwa mbele yako bila kuuliza maswali kwa ajili ya dhamiri.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama ukikaribishwa chakula na mtu asiyeamini nawe ukikubali kwenda, kula kila kitu kitakachowekwa mbele yako bila kuuliza maswali kwa ajili ya dhamiri.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mtu asiyeamini akiwaalika, nanyi mnataka kwenda, kuleni kila kitu kiwekwacho mbele yenu bila kuulizauliza, kwa ajili ya dhamiri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama mtu ambaye si mwaamini akiwaalikeni nanyi mkakubali kwenda, basi, kuleni vyote atakavyowaandalieni bila kuulizauliza kwa sababu ya dhamiri zenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtu asiyemtegemea Mungu akiwaalika, nanyi mkitaka kwenda, basi, vyote mnavyoandaliwa vileni pasipo kuuliza vitokapo mioyo isilemewe!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mtu asiyeamini akiwaalika, nanyi mnataka kwenda, kuleni kila kitu kiwekwacho mbele yenu bila kuuliza-uliza, kwa ajili ya dhamiri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama mupagani anawaalika kula chakula, nanyi mukikubali kwenda kule, mukule vyote wanavyotoa kwenu bila kuulizauliza neno kwa sababu ya zamiri.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na mtu asiyeamini akiwaalika, nanyi mnataka kwenda, kulani killa kitu kiwekwacho mbele yenu bila kuulizauliza, kwa ajili ya dhamiri.