1 Corinthians 10:28 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini mtu akiwaambieni: “Chakula hiki kimetambikiwa sanamu,” basi, kwa ajili ya huyo aliyewaambieni hivyo na kwa ajili ya dhamiri, msile.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini kama mtu yeyote akikuambia, “Hiki kimetolewa sadaka kwa sanamu,” basi usikile kwa ajili ya huyo aliyekuambia na kwa ajili ya dhamiri.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini mtu akiwaambia, Kitu hiki kimetolewa kiwe sadaka, msile, kwa ajili yake yeye aliyeonyesha, na kwa ajili ya dhamiri.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini mtu akiwaambia, “Chakula hicho kilitolewa sadaka katika hekalu la miungu,” basi msile. Kwa sababu kinaweza kumwathiri mtu na uhusiano wake na Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini mtu akiwaambieni: “Chakula hiki kimetambikiwa sanamu,” basi, kwa ajili ya huyo aliyewaambieni hivyo na kwa ajili ya dhamiri, msile.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini mtu akiwaambieni: “Chakula hiki kimetambikiwa sanamu,” basi, kwa ajili ya huyo aliyewaambieni hivyo na kwa ajili ya dhamiri, msile.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini kama mtu ye yote akikuambia, “Hiki kimetolewa kafara kwa sanamu,” basi usikile kwa ajili ya huyo aliyekuambia na kwa ajili ya dhamiri.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini kama mtu yeyote akikuambia, “Hiki kimetolewa kafara kwa sanamu,” basi usikile kwa ajili ya huyo aliyekuambia na kwa ajili ya dhamiri.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini mtu akiwaambia, Kitu hiki kimetolewa kiwe sadaka, msile, kwa ajili yake yeye aliyewaambia, na kwa ajili ya dhamiri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini mtu akiwaambieni: “Chakula hiki kimetambikiwa sanamu,” basi, kwa ajili ya huyo aliyewaambieni hivyo na kwa ajili ya dhamiri, msile.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini akiwaambia: Hii ni nyama ya tambiko, msiile kwa ajili yake yeye aliyewajulisha, tena kwa ajili ya mioyo isiyojua maana, isilemewe!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini mtu akiwaambia, Kitu hiki kimetolewa kiwe sadaka, msile, kwa ajili yake yeye aliyeonyesha, na kwa ajili ya dhamiri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kama mutu akiwaambia ninyi: “Vyakula hivi vimetambikiwa kwa sanamu,” basi musivikule kwa ajili ya yule aliyewaarifu na kwa ajili ya zamiri.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini mtu akiwaambieni, Kitu hiki kimetolewa sadaka kwa sanamu, msile, kwa ajili yake yeye aliyekuonyesha, na kwa ajili ya dhamiri; maana dunia ni mali ya Bwana na vitu vyote viijazavyo.