1 Corinthians 11:16 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama mtu anataka kuleta ubishi juu ya jambo hili, basi, na ajue kwamba sisi hatuna desturi nyingine, wala makanisa ya Mungu hayana desturi nyingine.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama mtu anataka kubishana kuhusu jambo hili, sisi wala makundi ya waumini ya Mungu hatutambui desturi nyingine.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini mtu ye yote akitaka kuleta fitina, sisi hatuna desturi kama hiyo, wala makanisa ya Mungu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baadhi ya watu wanaweza kuanzisha mabishano kuhusiana na yale niliyosema. Lakini desturi ambayo sisi na makanisa ya Mungu yanafuata ni hii: ya kwamba wanawake wanaweza kuomba na kutabiri ujumbe kutoka kwa Mungu, vichwa vyao vikiwa vimefunikwa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kama mtu anataka kuleta ubishi juu ya jambo hili, basi, na ajue kwamba sisi hatuna desturi nyingine, wala makanisa ya Mungu hayana desturi nyingine.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama mtu anataka kuleta ubishi juu ya jambo hili, basi, na ajue kwamba sisi hatuna desturi nyingine, wala makanisa ya Mungu hayana desturi nyingine.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama mtu anataka kubishana juu ya jambo hili, sisi wala makanisa ya Mungu hatutambui desturi nyingine.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama mtu anataka kubishana juu ya jambo hili, sisi wala makundi ya waumini ya Mungu hatutambui desturi nyingine.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini mtu yeyote akitaka kuleta fitina, sisi hatuna desturi kama hiyo, wala makanisa ya Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama mtu anataka kuleta ubishi juu ya jambo hili, basi, na ajue kwamba sisi hatuna desturi nyingine, wala makanisa ya Mungu hayana desturi nyingine.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini kama yuko anayependa mabisho, basi, mazoea kama hayo hayako wala kwetu wala po pote palipo na wateule wa Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini mtu ye yote akitaka kuleta fitina, sisi hatuna desturi kama hiyo, wala makanisa ya Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kama mutu akitaka kubishana juu ya neno hili, ajue kwamba sisi wala makanisa ya Mungu hatuna desturi ingine.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini mtu aliye yote, akitaka kuleta fitina, sisi hatuna desturi kama hiyo, wala makanisa ya Mungu.