1 Corinthians 11:18 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Awali ya yote, nasikia kwamba mnapokutana pamoja hutokea mafarakano kati yenu. Nami naamini kiasi,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwanza, mnapokutana kama kundi la waumini, nasikia kwamba kuna mgawanyiko miongoni mwenu, nami kwa kiasi fulani nasadiki kuwa ndivyo ilivyo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana kwanza mkutanikapo kanisani nasikia kuna faraka kwenu; nami nusu nasadiki;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwanza, nimesikia kuwa mnapokutana kama kanisa mmegawanyika. Hili si gumu kuliamini
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Awali ya yote, nasikia kwamba mnapokutana pamoja hutokea mafarakano kati yenu. Nami naamini kiasi,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Awali ya yote, nasikia kwamba mnapokutana pamoja hutokea mafarakano kati yenu. Nami naamini kiasi,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwanza, mnapokutana kama kanisa, nasikia kwamba kuna mgawanyiko miongoni mwenu, nami kwa kiasi fulani nasadiki kuwa ndivyo ilivyo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwanza, mnapokutana kama kundi la waumini, nasikia kwamba kuna mgawanyiko miongoni mwenu, nami kwa kiasi fulani nasadiki kuwa ndivyo ilivyo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana kwanza mnapokutanika kanisani nasikia kuna migawanyiko kwenu; nami kwa kiasi fulani naamini;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Awali ya yote, nasikia kwamba mnapokutana pamoja hutokea mafarakano kati yenu. Nami naamini kiasi,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani kwanza nasikia, ya kuwa hapo, mnapokutania wateule na wateule, yako magawanyiko, nami menginemengine nayasadiki.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana kwanza mkutanikapo kanisani nasikia kuna faraka kwenu; nami nusu nasadiki;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwanza, ninasikia kwamba munapokusanyika kuna matengano katikati yenu, nami ninasadiki kwamba nusu ya maneno yale ni ya kweli.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
kwa maana kwanza mkutanikapo kanisani nasikia kuna faraka kwenu; na nussu kidogo nasadiki: