1 Corinthians 11:2 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nawapeni hongera kwa sababu mnanikumbuka na kwa sababu mnayashikilia yale maagizo niliyowapeni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ninawasifu kwa kunikumbuka katika kila jambo na kwa kushika mapokeo kama nilivyowapatia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi nawasifu, kwa sababu mmenikumbuka katika mambo yote, nanyi mmeyashika yale mapokeo vile vile kama nilivyowatolea.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nawasifu kwa sababu daima mnanikumbuka mimi na kuyafuata mafundisho niliyowapa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nawapeni hongera kwa sababu mnanikumbuka na kwa sababu mnayashikilia yale maagizo niliyowapeni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nawapeni hongera kwa sababu mnanikumbuka na kwa sababu mnayashikilia yale maagizo niliyowapeni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ninawasifu kwa kuwa mnanikumbuka katika kila jambo na kwa kushika mafundisho niliyowapa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ninawasifu kwa kuwa mnanikumbuka katika kila jambo na kwa kushika mafundisho niliyowapa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi nawasifu, kwa sababu mmenikumbuka katika mambo yote, nanyi mmeyashika yale mapokeo vile vile kama nilivyowatolea.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nawapeni hongera kwa sababu mnanikumbuka na kwa sababu mnayashikilia yale maagizo niliyowapeni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nawasifu ninyi, ya kuwa mnanikumbuka po pote, mkashikamana nayo maagizo yangu, kama nilivyowaagiza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi nawasifu, kwa sababu mmenikumbuka katika mambo yote, nanyi mmeyashika yale mapokeo vile vile kama nilivyowatolea.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninawashukuru kwa sababu munanikumbuka katika mambo yote na kwa sababu munashika mafundisho yangu sawa vile nilivyoyafundisha kwenu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Tena nawasifu, ndugu, kwa sababu mmenikumbuka katika mambo yote, nanyi mmeyashika yale niliyowatolea vile vile kama nilivyowatolea.