1 Corinthians 11:22 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Je, hamwezi kula na kunywa nyumbani kwenu! Au je, mnalidharau kanisa la Mungu na kuwaaibisha hao wasio na kitu? Niwaambie nini? Niwasifu? La hasha! Si kuhusu jambo hili.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, hamna nyumbani kwenu ambako mnaweza kula na kunywa? Au mnalidharau kundi la waumini la Mungu na kuwadhalilisha wale wasio na kitu? Niwaambie nini? Je, niwasifu kuhusu jambo hili? La, hasha!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Je! Hamna nyumba za kulia na kunywea? Au mnalidharau kanisa la Mungu, na kuwatahayarisha hao wasio na kitu? Niwaambieni? Niwasifu? La! Siwasifu kwa ajili ya hayo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mnaweza kula na kunywa katika nyumba zenu. Inaonekana kuwa mnadhani kanisa la Mungu si muhimu. Mnawatahayarisha wasio na kitu. Niseme nini? Je, niwasifu? Hapana, siwezi kuwasifu katika hili.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Je, hamwezi kula na kunywa nyumbani kwenu! Au je, mnalidharau kanisa la Mungu na kuwaaibisha hao wasio na kitu? Niwaambie nini? Niwasifu? La hasha! Si kuhusu jambo hili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Je, hamwezi kula na kunywa nyumbani kwenu! Au je, mnalidharau kanisa la Mungu na kuwaaibisha hao wasio na kitu? Niwaambie nini? Niwasifu? La hasha! Si kuhusu jambo hili.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, hamna nyumbani kwenu ambako mnaweza kula na kunywa? Au mnalidharau kanisa la Mungu na kuwadhalilisha wale wasio na kitu? Niwaambie nini? Je, niwasifu juu ya jambo hili? La, hasha!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, hamna nyumbani kwenu ambako mnaweza kula na kunywa? Au mnalidharau kundi la waumini la Mungu na kuwadhalilisha wale wasio na kitu? Niwaambie nini? Je, niwasifu juu ya jambo hili? La, hasha!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Je! Hamna nyumba za kulia na kunywea? Au mnalidharau kanisa la Mungu, na kuwatahayarisha hao wasio na kitu? Niwaambieni? Niwasifu? La! Siwasifu kwa ajili ya hayo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Je, hamwezi kula na kunywa nyumbani kwenu! Au je, mnalidharau kanisa la Mungu na kuwaaibisha hao wasio na kitu? Niwaambie nini? Niwasifu? La hasha! Si kuhusu jambo hili.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Je, hamna nyumba zenu za kuliamo na kunyweamo? Au mwawabeza wateule wake Mungu mkiwatia soni wasio na kitu? Niwaambieje? Niwasifu? La! Katika hayo siwasifu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Je! Hamna nyumba za kulia na kunywea? Au mnalidharau kanisa la Mungu, na kuwatahayarisha hao wasio na kitu? Niwaambieni? Niwasifu? La! Siwasifu kwa ajili ya hayo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, ninyi hamuna nyumba munamoweza kukulia na kukunywea? Au munazarau kanisa la Mungu na munataka kuwapatisha haya wale wasiokuwa na kitu? Munataka niwaambie ninyi nini? Inafaa niwasifu? Hapana, siwezi kuwasifu hata kidogo juu ya jambo hilo!
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Je! hamna nyumba za kulia na kunywea? Au mnalidharau Kanisa la Mungu, na kuwatahayarisha wasio na kitu? Niwaambieni? niwasifu kwa haya? Siwasifu.