1 Corinthians 11:25 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Vivyo hivyo, baada ya kula, akatwaa kikombe cha divai, akasema: “Hiki ni kikombe cha agano jipya linalothibitishwa kwa damu yangu. Fanyeni hivi, kila mnapokunywa, kwa kunikumbuka.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Vivyo hivyo baada ya kula, akakitwaa kikombe, akisema, “Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu. Fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa namna hiyo hiyo, baada ya wote kula, Yesu alichukua kikombe cha divai na akasema, “Divai hii inawakilisha agano jipya ambalo Mungu anafanya na watu wake, linaloanza kwa sadaka ya damu yangu. Kila mnywapo divai hii, fanyeni hivi kwa ajili ya kunikumbuka mimi.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Vivyo hivyo, baada ya kula, akatwaa kikombe akasema: “Hiki ni kikombe cha agano jipya linalothibitishwa kwa damu yangu. Fanyeni hivi, kila mnapokunywa, kwa kunikumbuka.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Vivyo hivyo, baada ya kula, akatwaa kikombe cha divai, akasema: “Hiki ni kikombe cha agano jipya linalothibitishwa kwa damu yangu. Fanyeni hivi, kila mnapokunywa, kwa kunikumbuka.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Vivi hivi baada ya kula, akakitwaa kikombe, akisema, “Kikombe hiki ni Agano jipya katika damu yangu. Fanyeni hivi kila mnywapo kwa ukumbusho wangu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Vivyo hivyo baada ya kula, akakitwaa kikombe, akisema, “Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu. Fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Vivyo hivyo, baada ya kula, akatwaa kikombe cha divai, akasema: “Hiki ni kikombe cha agano jipya linalothibitishwa kwa damu yangu. Fanyeni hivi, kila mnapokunywa, kwa kunikumbuka.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Vivyo hivyo akakitwaa nacho kinyweo, walipokwisha kula, akisema: Kinyweo hiki ndicho Agano Jipya katika damu yangu. Fanyizeni hivyo, kila mtakapokinywea, mnikumbuke!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vilevile, nyuma ya kula akatwaa kikombe na kusema: “Kikombe hiki ni agano jipya la Mungu, linalohakikishwa kwa njia ya damu yangu. Mufanye hivi kwa kunikumbuka kila mara munapokikunywa.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Vivi hivi nacho kikombe baada ya kula, akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu: fanyeni liivi killa mnywapo, kwa ukumbusho wangu.