1 Corinthians 11:4 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, kila mwanamume anayesali au anayetangaza ujumbe wa Mungu huku amefunika kichwa chake, huyo anamdharau Kristo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kila mwanaume anayeomba au kutoa unabii akiwa amefunika kichwa chake, anakiaibisha kichwa chake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kila mwanamume, asalipo, au anapohutubu, naye amefunikwa kichwa, yuaaibisha kichwa chake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kila mwanaume anayeomba au kutabiri akiwa amefunika kichwa chake, anakiaibisha kichwa chake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, kila mwanamume anayesali au anayetangaza ujumbe wa Mungu huku amefunika kichwa chake, huyo anamdharau Kristo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, kila mwanamume anayesali au anayetangaza ujumbe wa Mungu huku amefunika kichwa chake, huyo anamdharau Kristo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kila mwanaume anayeomba au kutoa unabii akiwa amefunika kichwa chake, anakiaibisha kichwa chake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kila mwanaume anayeomba au kutoa unabii akiwa amefunika kichwa chake, anakiaibisha kichwa chake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kila mwanamume, asalipo, au anapotoa unabii, naye amefunikwa kichwa, anaaibisha kichwa chake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, kila mwanamume anayesali au anayetangaza ujumbe wa Mungu huku amefunika kichwa chake, huyo anamdharau Kristo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kila mume akiomba au akifumbua Neno na kuvaa kichwani, hukipatia kichwa chake soni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kila mwanamume, asalipo, au anapohutubu, naye amefunikwa kichwa, yuaaibisha kichwa chake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi mwanaume yeyote akifunika kichwa chake wakati anapoomba Mungu, au anapotabiri, anamuzaraulisha Kristo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Killa mwanamume, asalipo, au atoapo unabii, nae ana kitu kichwani, yuaibisha kichwa chake.