1 Corinthians 11:6 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwanamke asiyefunika kichwa chake, afadhali anyoe nywele zake. Lakini ni aibu kwa mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa; basi, afadhali afunike kichwa chake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama mwanamke hatajifunika kichwa chake, basi inampasa kunyoa nywele zake. Lakini kama ni aibu kwa mwanamke kukata au kunyoa nywele zake, basi afunike kichwa chake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana mwanamke asipofunikwa na akatwe nywele. Au ikiwa ni aibu mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa, na afunikwe.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ikiwa mwanamke hatafunika kichwa chake, basi na azinyoe nywele zake. Lakini ni aibu kwa mwanamke kukata nywele zake au kuzinyoa kichwani mwake. Hivyo anapaswa kufunika kichwa chake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mwanamke asiyefunika kichwa chake, afadhali anyoe nywele zake. Lakini ni aibu kwa mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa; basi, afadhali afunike kichwa chake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwanamke asiyefunika kichwa chake, afadhali anyoe nywele zake. Lakini ni aibu kwa mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa; basi, afadhali afunike kichwa chake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama mwanamke hatajifunika kichwa chake, basi inampasa kunyoa nywele zake. Lakini kama ni aibu kwa mwanamke kunyoa nywele zake, basi afunike kichwa chake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama mwanamke hatajifunika kichwa chake, basi inampasa kunyoa nywele zake. Lakini kama ni aibu kwa mwanamke kukata au kunyoa nywele zake, basi afunike kichwa chake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana mwanamke asipojifunika kichwa, na akatwe nywele. Au ikiwa ni aibu mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa, na afunike kichwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwanamke asiyefunika kichwa chake, afadhali anyoe nywele zake. Lakini ni aibu kwa mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa; basi, afadhali afunike kichwa chake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Maana mke asipovaa kichwani, naye akatwe nywele! Lakini mke akiona soni ya kukatwa nyuwele au kunyolewa avae kichwani!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana mwanamke asipofunikwa na akatwe nywele. Au ikiwa ni aibu mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa, na afunikwe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama mwanamuke hafuniki kichwa, anaweza basi kunyolewa! Lakini kwa sababu ni haya kwa mwanamuke kukatwa nywele au kunyolewa, basi inafaa afunike kichwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana mwanamke asipofunikwa na anyoe. Au ikiwa ni unyonge mwanamke akate nywele zake au kunyoa, na afunikwe.