1 Corinthians 12:16 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama sikio lingejisemea: “Kwa vile mimi si jicho, basi mimi si mali ya mwili,” je, kwa hoja hiyo lingekoma kuwa sehemu ya mwili? La!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Na kama sikio lingesema, “Kwa kuwa mimi si jicho, basi mimi si wa mwili,” hiyo isingefanya hilo sikio lisiwe sehemu ya mwili.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na sikio likisema, Kwa kuwa mimi si jicho, mimi si la mwili; je! Si la mwili kwa sababu hiyo?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Sikio linaweza kusema, “Mimi si jicho, hivyo mimi si wa mwili.” Lakini kwa kusema hivi hakutafanya sikio lisiwe kiungo cha mwili.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kama sikio lingejisemea: “Kwa vile mimi si jicho, basi mimi si mali ya mwili”, je, kwa hoja hiyo lingekoma kuwa sehemu ya mwili? La!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama sikio lingejisemea: “Kwa vile mimi si jicho, basi mimi si mali ya mwili,” je, kwa hoja hiyo lingekoma kuwa sehemu ya mwili? La!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Na kama sikio lingesema, “Kwa kuwa mimi si jicho, basi mimi si la mwili,” hiyo isingefanya hilo sikio lisiwe sehemu ya mwili.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Na kama sikio lingesema, “Kwa kuwa mimi si jicho, basi mimi si wa mwili,” hiyo isingefanya hilo sikio lisiwe sehemu ya mwili.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na sikio likisema, Kwa kuwa mimi si jicho, mimi si wa mwili; je! Linakuwa si la mwili kwa sababu hiyo?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama sikio lingejisemea: “Kwa vile mimi si jicho, basi mimi si mali ya mwili,” je, kwa hoja hiyo lingekoma kuwa sehemu ya mwili? La!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nalo sikio likisema: Kwa sababu si jicho, mimi si la mwili je? Kwa hiyo silo la mwili?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na sikio likisema, Kwa kuwa mimi si jicho, mimi si la mwili; je! Si la mwili kwa sababu hiyo?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na kama sikio lingesema: “Kwa sababu mimi si jicho, basi mimi si wa mwili,” hata vile halingeacha kuwa kiungo cha mwili.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na sikio likisema, Mimi si jicho, mimi si wa mwili; je! si wa mwili kwa sababu hiyo?