1 Corinthians 12:23 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tena, viungo vile tunavyovifikiria kuwa havistahili heshima kubwa, ndivyo tunavyovitunza kwa uangalifu zaidi; viungo vya mwili ambavyo havionekani kuwa vizuri sana, huhifadhiwa zaidi,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Navyo vile viungo tunavyoviona havina heshima, ndivyo tunavipa heshima maalum. Vile viungo vya mwili ambavyo havina uzuri, tunavipa heshima ya pekee;
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa havina heshima, viungo vile twavipa heshima zaidi; na viungo vyetu visivyo na uzuri vina uzuri zaidi sana.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na viungo ambavyo tunadhani kuwa vina umuhimu mdogo ndivyo tunavitunza kwa heshima kubwa. Na tunavitunza kwa kuvifunika kwa uangalifu maalum viungo vya mwili tusivyotaka kuvionesha.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Tena, viungo vile tunavyovifikiria kuwa havistahili heshima kubwa, ndivyo tunavyovitunza kwa uangalifu zaidi; viungo vya mwili ambavyo havionekani kuwa vizuri sana, huhifadhiwa zaidi,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tena, viungo vile tunavyovifikiria kuwa havistahili heshima kubwa, ndivyo tunavyovitunza kwa uangalifu zaidi; viungo vya mwili ambavyo havionekani kuwa vizuri sana, huhifadhiwa zaidi,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Navyo vile viungo vya mwili tunavyoviona havina heshima, ndivyo tunavipa heshima maalum. Vile viungo vya mwili ambavyo havina uzuri, tunavipa heshima ya pekee.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Navyo vile viungo tunavyoviona havina heshima, ndivyo tunavipa heshima maalum. Vile viungo vya mwili ambavyo havina uzuri, tunavipa heshima ya pekee;
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa havina heshima, viungo vile tunavipa heshima zaidi; na viungo vyetu visivyo na uzuri vina uzuri zaidi sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tena, viungo vile tunavyovifikiria kuwa havistahili heshima kubwa, ndivyo tunavyovitunza kwa uangalifu zaidi; viungo vya mwili ambavyo havionekani kuwa vizuri sana, huhifadhiwa zaidi,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Navyo, tunavyoviwazia kuwa vyenye soni, hupata heshima kuliko vingine; navyo visivyo vizuri hupambwa kuliko vingine.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa havina heshima, viungo vile twavipa heshima zaidi; na viungo vyetu visivyo na uzuri vina uzuri zaidi sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena viungo vile tunavyozania kwamba havistahili heshima kubwa ndivyo tunavyoheshimu zaidi. Na viungo vinavyokuwa vya haya ndivyo tunavyotunza sana,
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na vile vidhaniwavyo kuwa havina heshima, viungo vile twavipa heshima zaidi; na viungo vyetu visivyo na uzuri vina uzuri zaidi sana.