1 Corinthians 12:26 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama kiungo kimoja kinaumia viungo vyote huumia pamoja nacho. Kiungo kimoja kikisifiwa viungo vingine vyote hufurahi pamoja nacho.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia pamoja nacho; kama kiungo kimoja kikipewa heshima, viungo vyote hufurahi pamoja nacho.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia nacho, na kiungo kimoja kikitukuzwa, viungo vyote hufurahi pamoja nacho.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ikiwa kiungo kimoja cha mwili kinaugua, basi viungo vyote vinaugua pamoja nacho. Au ikiwa kiungo kimoja kinaheshimiwa, basi viungo vingine vyote vinashiriki heshima ya kiungo hicho.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kama kiungo kimoja kinaumia viungo vyote huumia pamoja nacho. Kiungo kimoja kikisifiwa viungo vingine vyote hufurahi pamoja nacho.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama kiungo kimoja kinaumia viungo vyote huumia pamoja nacho. Kiungo kimoja kikisifiwa viungo vingine vyote hufurahi pamoja nacho.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia pamoja nacho, kama kiungo kimoja kikipewa heshima, viungo vyote hufurahi pamoja nacho.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia pamoja nacho, kama kiungo kimoja kikipewa heshima, viungo vyote hufurahi pamoja nacho.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia nacho, na kiungo kimoja kikitukuzwa, viungo vyote hufurahi pamoja nacho.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama kiungo kimoja kinaumia viungo vyote huumia pamoja nacho. Kiungo kimoja kikisifiwa viungo vingine vyote hufurahi pamoja nacho.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Napo kiungo kimoja kinapoumia, basi, viungo vyote huumia pamoja nacho; napo kiungo kimoja kinapotukuzwa, basi, viungo vyote hufurahi pamoja nacho.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia nacho, na kiungo kimoja kikitukuzwa, viungo vyote hufurahi pamoja nacho.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama kiungo kimoja kikiumia, viungo vingine vyote vinaugua pamoja nacho. Kiungo kimoja kikiheshimiwa, viungo vingine vyote vinafurahi pamoja nacho.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia navyo, na kiungo kimoja kikitukuzwa, viungo vyote hufurahi pamoja.