1 Corinthians 12:28 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mungu ameweka katika kanisa: Kwanza mitume, pili manabii, tatu waalimu; kisha ameweka wale wenye kipaji cha kufanya miujiza, kuponya na kusaidia; viongozi na wenye kusema lugha ngeni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mungu ameweka katika jumuiya ya waumini kwanza mitume, pili manabii, tatu walimu, kisha watenda miujiza, pia karama za kuponya, karama za kusaidiana, karama za uongozi, na aina mbalimbali za lugha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lugha.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na Mungu ameweka katika kanisa, kwanza, baadhi kuwa mitume, pili manabii, na tatu walimu. Kisha Mungu ametoa nafasi kwa wale wanaofanya miujiza, wenye karama ya uponyaji, wanaoweza kuwasaidia wengine, wanaoweza kuwaongoza wengine na wale wanaoweza kuzungumza kwa lugha zingine.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mungu ameweka katika kanisa: kwanza mitume, pili manabii, tatu walimu; kisha ameweka wale wenye kipaji cha kufanya miujiza, kuponya, kusaidia; viongozi na wenye kusema lugha ngeni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mungu ameweka katika kanisa: kwanza mitume, pili manabii, tatu waalimu; kisha ameweka wale wenye kipaji cha kufanya miujiza, kuponya na kusaidia; viongozi na wenye kusema lugha ngeni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mungu ameweka katika kanisa, kwanza mitume, pili manabii, tatu walimu, kisha watenda miujiza, pia karama za kuponya, karama za masaidiano, karama za maongozi, aina mbalimbali za lugha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mungu ameweka katika jumuiya ya waumini kwanza mitume, pili manabii, tatu walimu, kisha watenda miujiza, pia karama za kuponya, karama za kusaidiana, karama za uongozi, aina mbalimbali za lugha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na Mungu ameweka wengine katika kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, aina za usaidizi, maongozi na aina za lugha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mungu ameweka katika kanisa: Kwanza mitume, pili manabii, tatu waalimu; kisha ameweka wale wenye kipaji cha kufanya miujiza, kuponya na kusaidia; viongozi na wenye kusema lugha ngeni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wako, Mungu aliowawekea wateule: kwanza mitume, wa pili wafumbuaji, wa tatu wafunzi, kisha wenye nguvu, kisha wenye magawio ya kuponya wagonjwa nao watumikizi nao wenye kuongoza nao wenye misemo migeni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lugha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vilevile Mungu ameweka kwanza mitume katika kanisa; pili manabii na tatu walimu; kisha kunakuwa wale wenye zawadi ya kufanya miujiza, ya kuponyesha wagonjwa, ya kusaidia wengine, ya kuongoza wengine, ya kusema luga za ajabu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kiisha miujiza, kiisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na kutawala, na aina za lugha.