1 Corinthians 13:1 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hata kama nikinena lugha za watu na hata za malaika, lakini kama sina upendo mimi nimekuwa tu kama sauti ya debe tupu au kengele.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hata kama nikisema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa kengele inayolia au toazi linalovuma.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ninaweza kusema kwa lugha zingine, za wanadamu au za malaika. Lakini ikiwa sina upendo, mimi ni kengele yenye kelele na tuazi linalolia.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hata kama nikinena lugha za watu na hata za malaika, lakini kama sina upendo mimi nimekuwa tu kama sauti ya debe tupu au kengele.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hata kama nikinena lugha za watu na hata za malaika, lakini kama sina upendo mimi nimekuwa tu kama sauti ya debe tupu au kengele.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hata kama nitasema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa kengele inayolialia au toazi livumalo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hata kama nitasema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa kengele inayolialia au toazi livumalo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hata kama nikinena lugha za watu na hata za malaika, lakini kama sina upendo mimi nimekuwa tu kama sauti ya debe tupu au kengele.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Ijapo niseme misemo ya kimtu na ya kimalaika, nisipokuwa na upendo, ndimi upatu wenye milio au njuga yenye makelele.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hata nikiwa na uwezo wa kusema luga za watu na za wamalaika, lakini kama sina upendo, masemi yangu ni bure kama vile kelele la kengele au matoazi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
NIJAPOSEMA kwa lugha za wana Adamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upato uvumao.