1 Corinthians 14:1 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Jitahidini kuwa na upendo. Vilevile fanyeni bidii ya kupata vipaji vingine vya kiroho, hasa kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Fuateni upendo na kutaka sana karama za roho, hasa karama ya unabii.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ufuateni upendo, na kutaka sana karama za rohoni, lakini zaidi kwamba mpate kuhutubu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Upendo uwe lengo la maisha yenu, lakini mnapaswa pia kuzitaka karama za Roho. Na itakeni sana karama ya unabii.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Jitahidini kuwa na upendo. Vilevile fanyeni bidii ya kupata vipaji vingine vya kiroho, hasa kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Jitahidini kuwa na upendo. Vilevile fanyeni bidii ya kupata vipaji vingine vya kiroho, hasa kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Fuateni upendo na kutaka sana karama za roho, hasa karama ya unabii.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Fuateni upendo na kutaka sana karama za roho, hasa karama ya unabii.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ufuatilieni upendo, na kutaka sana karama za rohoni, lakini zaidi kwamba mpate kutoa unabii.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Jitahidini kuwa na upendo. Vilevile fanyeni bidii ya kupata vipaji vingine vya kiroho, hasa kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ukimbilieni upendo! Jikazeni, myapate ya Kiroho, kupita mengine, mweze kufumbua!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ufuateni upendo, na kutaka sana karama za rohoni, lakini zaidi kwamba mpate kuhutubu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mujikaze mukuwe na upendo. Vilevile mutamani sana kupata zawadi za Roho, hasa zaidi zawadi ya kutabiri.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
UFUATIENI upendo, katakeni sana karama za rohoni, lakini zaidi mpate kukhutubu.