1 Corinthians 14:11 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini ikiwa mimi sifahamu maana ya lugha asemayo mtu fulani, mimi ni mgeni kwake mtu huyo naye pia ni mgeni kwangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi kama sielewi maana ya hiyo sauti, nitakuwa mgeni kwa yule msemaji, naye atakuwa mgeni kwangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi nisipoijua maana ya ile sauti nitakuwa kama mjinga kwake yeye anenaye; naye anenaye atakuwa mjinga kwangu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini ikiwa sielewi maana ya maneno wanayosema wengine, kwangu itakuwa sauti ya ajabu tu, na nitasikika kama ninayetoa sauti za ajabu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini ikiwa mimi sifahamu maana ya lugha asemayo mtu fulani, mimi ni mgeni kwake mtu huyo naye pia ni mgeni kwangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini ikiwa mimi sifahamu maana ya lugha asemayo mtu fulani, mimi ni mgeni kwake mtu huyo naye pia ni mgeni kwangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi kama sielewi maana ya hiyo sauti, nitakuwa mgeni kwa yule msemaji, naye atakuwa mgeni kwangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi kama sielewi maana ya hiyo sauti, nitakuwa mgeni kwa yule msemaji, naye atakuwa mgeni kwangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi nisipoijua maana ya ile sauti nitakuwa kama mjinga kwake yeye anenaye; naye anenaye atakuwa mjinga kwangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini ikiwa mimi sifahamu maana ya lugha asemayo mtu fulani, mimi ni mgeni kwake mtu huyo naye pia ni mgeni kwangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nisipoijua maana ya msemo, nitakuwa kama mjinga kwake yeye anayeusema, naye asemaye atakuwa mjinga kwangu mimi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi nisipoijua maana ya ile sauti nitakuwa kama mjinga kwake yeye anenaye; naye anenaye atakuwa mjinga kwangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi kama nisipojua luga fulani, nitakuwa kama mujinga kwa yule anayeisema, naye atakuwa kama mujinga kwangu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi nisipojua maana ya ile sauti nitakuwa mshenzi kwake yeye anenae; nae atakuwa mshenzi kwangu.