1 Corinthians 14:19 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini katika mikutano ya waumini napendelea zaidi kusema maneno matano yenye kueleweka ili niwafundishe wengine, kuliko kusema maneno elfu ya lugha ngeni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini katika kundi la waumini ni afadhali niseme maneno matano ya kueleweka ili niwafundishe wengine kuliko kusema maneno elfu kumi kwa lugha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
lakini katika kanisa napenda kunena maneno matano kwa akili zangu, nipate kuwafundisha wengine, zaidi ya kunena maneno kumi elfu kwa lugha.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini wakati wa mikutano ya kanisa napenda kuzungumza maneno matano ninayoyaelewa kuliko maelfu ya maneno katika lugha zingine. Ni afadhali nizungumze nikiwa katika uelewa wangu ili niwafundishe wengine.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini katika mikutano ya waumini napendelea zaidi kusema maneno matano yenye kueleweka ili niwafundishe wengine, kuliko kusema maneno elfu ya lugha ngeni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini katika mikutano ya waumini napendelea zaidi kusema maneno matano yenye kueleweka ili niwafundishe wengine, kuliko kusema maneno elfu ya lugha ngeni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini ndani ya kanisa ni afadhali niseme maneno matano ya kueleweka kwa akili ili niwafundishe wengine kuliko kusema maneno 10,000 kwa lugha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini ndani ya kanisa ni afadhali niseme maneno matano ya kueleweka ili niwafundishe wengine kuliko kusema maneno 10,000 kwa lugha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
lakini katika kanisa napenda kunena maneno matano kwa akili zangu, nipate kuwafundisha wengine, kuliko kunena maneno elfu kumi kwa lugha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini katika mikutano ya waumini napendelea zaidi kusema maneno matano yenye kueleweka ili niwafundishe wengine, kuliko kusema maneno elfu ya lugha ngeni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini kwenye wateule kusema maneno matano tu na kuyawaza, kwamba niwafundishe hata wengine, kwanipendeza kuliko kusema maneno elfu kumi kwa hiyo misemo migeni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
lakini katika kanisa napenda kunena maneno matano kwa akili zangu, nipate kuwafundisha wengine, zaidi ya kunena maneno kumi elfu kwa lugha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini, katika mukutano ninapenda kusema maneno matano yenye kusikilika, kusudi niwafundishe wengine, kuliko kusema maneno elfu kumi kwa luga za ajabu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
lakini napenda kunena maneno matano katika kanisa kwa akili zangu, nipate kuwafundisha wengine, zaidi ya kunena maneno elfu kumi kwa lugha.