1 Corinthians 14:20 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndugu, msiwe kama watoto katika fikira zenu. Kuhusu uovu, muwe kama watoto wachanga, lakini katika kufikiri ni lazima muwe kama watu waliokomaa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndugu zangu, msiwe kama watoto katika kufikiri kwenu, afadhali kuhusu uovu mwe kama watoto wachanga, lakini katika kufikiri kwenu, mwe watu wazima.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndugu zangu, msiwe watoto katika akili zenu; lakini katika uovu mgeuzwe watoto wachanga, bali katika akili zenu mkawe watu wazima.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndugu zangu, msiwaze kama watoto wadogo. Iweni kama watoto wachanga katika mambo maovu, lakini katika kuwaza kwenu muwe kama watu wazima, waliokua.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ndugu, msiwe kama watoto katika fikira zenu. Kuhusu uovu muwe kama watoto wachanga lakini katika kufikiri ni lazima muwe kama watu waliokomaa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndugu, msiwe kama watoto katika fikira zenu. Kuhusu uovu, muwe kama watoto wachanga, lakini katika kufikiri ni lazima muwe kama watu waliokomaa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndugu zangu, msiwe kama watoto katika kufikiri kwenu, afadhali kuhusu uovu mwe kama watoto wachanga, lakini katika kufikiri kwenu, mwe watu wazima.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndugu zangu, msiwe kama watoto katika kufikiri kwenu, afadhali kuhusu uovu mwe kama watoto wachanga, lakini katika kufikiri kwenu, mwe watu wazima.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndugu zangu, msiwe watoto katika akili zenu; lakini katika uovu mgeuzwe watoto wachanga, bali katika akili zenu muwe watu wazima.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndugu, msiwe kama watoto katika fikira zenu. Kuhusu uovu, muwe kama watoto wachanga, lakini katika kufikiri ni lazima muwe kama watu waliokomaa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndugu, mawazo yenu yasiwe ya kitoto, ila uovu tu mfanane na vitoto vichanga! Lakini mawazo yenu sharti yawe ya watu wazima!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndugu zangu, msiwe watoto katika akili zenu; lakini katika uovu mgeuzwe watoto wachanga, bali katika akili zenu mkawe watu wazima.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wandugu zangu, musikuwe kama watoto kwa kufikiri: lakini katika mambo mabaya, iwatokee kutenda kama watoto wachanga. Inafaa mafikiri yenu yakuwe kama ya watu wazima.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ndugu, msiwe watoto katika akili zenu; illakini katika uovu mwe watoto wachanga, bali katika akili zenu mwe watu wazima.