1 Corinthians 14:21 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Imeandikwa katika sheria: “Bwana asema hivi: ‘Kwa njia ya wenye kunena lugha ngeni, na kwa midomo ya wageni, nitasema na watu hawa, hata hivyo, hawatanisikiliza.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika Torati imeandikwa kwamba: “Kupitia kwa watu wenye lugha ng’eni na kupitia midomo ya wageni, nitasema na watu hawa, lakini hata hivyo hawatanisikiliza, asema Mwenyezi Mungu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Imeandikwa katika torati, Nitasema na watu hawa kwa watu wa lugha nyingine, na kwa midomo ya wageni, wala hata hivyo hawatanisikia, asema Bwana.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kama Maandiko yanavyosema, “Kwa kutumia wanaozungumza lugha tofauti na kutumia midomo ya wageni, nitazungumza na watu hawa, hata hivyo, hawatanitii.” Hivi ndivyo Bwana anasema.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Imeandikwa katika Sheria: “Bwana asema hivi: Kwa njia ya wenye kunena lugha ngeni, na kwa midomo ya wageni, nitasema na watu hawa, hata hivyo, hawatanisikiliza.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Imeandikwa katika sheria: “Bwana asema hivi: ‘Kwa njia ya wenye kunena lugha ngeni, na kwa midomo ya wageni, nitasema na watu hawa, hata hivyo, hawatanisikiliza.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika sheria imeandikwa kwamba: “Kwa kupitia watu wenye lugha ngeni na kupitia midomo ya watu wageni, nitasema na watu hawa, lakini hata hivyo hawatanisikiliza,” asema Bwana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika Torati imeandikwa kwamba: “Kupitia kwa watu wenye lugha ng’eni na kupitia midomo ya wageni, nitasema na watu hawa, lakini hata hivyo hawatanisikiliza,” asema Bwana Mwenyezi Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Imeandikwa katika torati, Nitasema na watu hawa kwa watu wa lugha nyingine, na kwa midomo ya wageni, wala hata hivyo hawatanisikia, asema Bwana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Imeandikwa katika sheria: “Bwana asema hivi: ‘Kwa njia ya wenye kunena lugha ngeni, na kwa midomo ya wageni, nitasema na watu hawa, hata hivyo, hawatanisikiliza.’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Katika Maonyo imeandikwa: Ukoo huu nitasema nao misemo migeni kwa midomo migeni, lakini hata hivyo hawatanisikia; ndivyo, asemavyo Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Imeandikwa katika torati, Nitasema na watu hawa kwa watu wa lugha nyingine, na kwa midomo ya wageni, wala hata hivyo hawatanisikia, asema Bwana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Imeandikwa katika Sheria: “Bwana anasema: ‘Nitasema na watu hawa kwa njia ya wageni wenye luga ngeni Na hata hivi hawatanisikiliza.’ ”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Imeandikwa katika torati ya kama, Nitanena na watu hawa kwa watu wa lugha nyingine, na kwa midomo ya wageni, na hatta hivi hawatanisikia, asema Bwana.