1 Corinthians 14:22 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo basi, kipaji cha kusema lugha ngeni ni ishara, si kwa ajili ya watu wenye imani, bali kwa ajili ya wale wasioamini; lakini kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu ni kwa ajili ya wale wanaoamini na si kwa ajili ya wasioamini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi kunena kwa lugha ni ishara, si kwa waaminio, bali kwa wasioamini, wakati unabii si kwa ajili ya wasioamini, bali kwa ajili ya waaminio.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, hizi lugha ni ishara, si kwao waaminio, bali kwao wasioamini lakini kuhutubu si kwa ajili yao wasioamini, bali kwa ajili yao waaminio.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na kutokana na hili tunaona kwamba matumizi ya lugha zingine ni ishara kuonesha namna ambavyo Mungu anawashughulikia wasioamini, na si walioamini. Na unabii unaonesha namna ambavyo Mungu hutenda kazi kupitia wanaoamini, na si wasioamini.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hivyo basi, kipaji cha kusema lugha ngeni ni ishara, si kwa ajili ya watu wenye imani, bali kwa ajili ya wale wasioamini; lakini kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu ni kwa ajili ya wale wanaoamini na si kwa ajili ya wasioamini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo basi, kipaji cha kusema lugha ngeni ni ishara, si kwa ajili ya watu wenye imani, bali kwa ajili ya wale wasioamini; lakini kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu ni kwa ajili ya wale wanaoamini na si kwa ajili ya wasioamini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi kunena kwa lugha mpya ni ishara, si kwa watu waaminio, bali kwa ajili ya wasioamini, wakati unabii si kwa ajili ya wasioamini, bali kwa ajili ya waaminio.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi kunena kwa lugha ni ishara, si kwa watu waaminio, bali kwa wasioamini, wakati unabii si kwa ajili ya wasioamini, bali kwa ajili ya waaminio.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, hizi lugha ni ishara, si kwao waaminio, bali kwao wasioamini lakini kutoa unabii si kwa ajili yao wasioamini, bali kwa ajili yao waaminio.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo basi, kipaji cha kusema lugha ngeni ni ishara, si kwa ajili ya watu wenye imani, bali kwa ajili ya wale wasioamini; lakini kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu ni kwa ajili ya wale wanaoamini na si kwa ajili ya wasioamini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo ile misemo migeni ni kielekezo, lakini si kwao wamtegemeao Bwana, ila kwao wakataao kumtegemea; lakini ufumbuaji nao ni kielekezo, lakini si kwao wakataao kumtegemea, ila kwao wamtegemeao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, hizi lugha ni ishara, si kwao waaminio, bali kwao wasioamini lakini kuhutubu si kwa ajili yao wasioamini, bali kwa ajili yao waaminio.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo, zawadi ya kusema luga za ajabu ni kitambulisho kwa wasioamini, lakini si kwa waamini. Na zawadi ya kutabiri ni kitambulisho kwa waamini, lakini si kwa wasioamini.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi, lugha ni ishara, si kwao waaminio, bali kwao wasioamini. Lakini kukhutuhu si kwa ajili yao wasioamini, bali kwa ajili yao waaminio.