1 Corinthians 14:23 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, kanisa lote linapokutana pamoja, na wote wakaanza kusema kwa lugha ngeni, kama wakija watu wa kawaida au wasioamini, je, hawatasema kwamba nyinyi mna wazimu?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo kama kundi la waumini wote wakikutana na kila mmoja akanena kwa lugha, kisha wakaingia wageni wasioelewa au wasioamini, je, hawatasema kwamba wote mna wazimu?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Haya! Ikiwa kanisa lote limekusanyika pamoja, na wote wanene kwa lugha, kisha ikawa wameingia watu wajinga au wasioamini, je! Hawatasema ya kwamba mna wazimu?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Chukulieni kuwa kanisa lote limekusanyika nanyi nyote mkaanza kusema kwa lugha zingine. Ikiwa baadhi ya watu wasio sehemu ya kundi lenu au wasio waamini wataingia katika kusanyiko lenu, watasema ninyi ni wendawazimu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, kanisa lote linapokutana pamoja, na wote wakaanza kusema kwa lugha ngeni, kama wakija watu wa kawaida au wasioamini, je, hawatasema kwamba ninyi mna wazimu?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, kanisa lote linapokutana pamoja, na wote wakaanza kusema kwa lugha ngeni, kama wakija watu wa kawaida au wasioamini, je, hawatasema kwamba nyinyi mna wazimu?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo kama kanisa lote likikutana na kila mmoja akanena kwa lugha, kisha wakaingia wageni wasioamini, je, hawatasema kwamba wote mna wazimu?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo kama kundi la waumini lote likikutana na kila mmoja akanena kwa lugha, kisha wakaingia wageni wasioelewa au wasioamini, je, hawatasema kwamba wote mna wazimu?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Haya! Ikiwa kanisa lote limekusanyika pamoja, na wote wanene kwa lugha, kisha ikawa wameingia watu wajinga au wasioamini, je! Hawatasema ya kwamba mna wazimu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, kanisa lote linapokutana pamoja, na wote wakaanza kusema kwa lugha ngeni, kama wakija watu wa kawaida au wasioamini, je, hawatasema kwamba nyinyi mna wazimu?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama wateule wote wanakusanyika pamoja, wote wakasema misemo migeni, tena pakiingia watu waliopumbaa au wasiomtegemea Bwana, je? Hawatasema: Mna wazimu?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Haya! Ikiwa kanisa lote limekusanyika pamoja, na wote wanene kwa lugha, kisha ikawa wameingia watu wajinga au wasioamini, je! Hawatasema ya kwamba mna wazimu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi kama kanisa zima limekusanyika, na watu wote wanaanza kusema kwa luga za ajabu; na kisha watu wasioelewa kitu au wasioamini wakiingia katika mukutano wenu hawatasema kuwa ninyi ni wenda-wazimu?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi ikiwa kanisa lote limekusanyika pamoja, na wote wananena kwa lugha, kiisha wakaingia watu wajinga au wasioamini, je! hawatasema ya kwamba mna wazimu?