1 Corinthians 14:26 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndugu, tuseme nini, basi? Mnapokutana pamoja, mmoja aimbe wimbo, mwingine atoe mafundisho, mwingine awe na ufunuo kutoka kwa Mungu, mwingine atumie kipaji cha kusema kwa lugha ngeni na mwingine afafanue yanayosemwa. Yote yawe kwa ajili ya kulijenga kanisa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi tuseme nini ndugu zangu? Mnapokutana pamoja, kila mmoja ana wimbo, au neno la mafundisho, au ufunuo, lugha mpya au atatafsiri. Mambo yote yatendeke kwa ajili ya kulijenga kundi la waumini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, ndugu, imekuwaje? Mkutanapo pamoja, kila mmoja ana zaburi, ana fundisho, ana ufunuo, ana lugha, ana tafsiri. Mambo yote na yatendeke kwa kusudi la kujenga.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Basi ndugu, mnapaswa kufanya nini? Mnapokusanyika, mtu mmoja ana wimbo, mwingine ana mafundisho na mwingine ana kweli mpya kutoka kwa Mungu. Mmoja anasema kwa lugha nyingine na mwingine anafasiri lugha hiyo. Cho chote mnachofanya lazima kiwe na lengo la kumfanya kila mmoja wenu akue katika imani.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ndugu, tuseme nini, basi? Mnapokutana pamoja, mmoja aimbe wimbo, mwingine atoe mafundisho, mwingine awe na ufunuo kutoka kwa Mungu, mwingine atumie kipaji cha kusema kwa lugha ngeni na mwingine afafanue yanayosemwa. Yote yawe kwa ajili ya kulijenga kanisa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndugu, tuseme nini, basi? Mnapokutana pamoja, mmoja aimbe wimbo, mwingine atoe mafundisho, mwingine awe na ufunuo kutoka kwa Mungu, mwingine atumie kipaji cha kusema kwa lugha ngeni na mwingine afafanue yanayosemwa. Yote yawe kwa ajili ya kulijenga kanisa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi tuseme nini ndugu zangu? Mnapokutana pamoja, mmoja ana wimbo, mwingine neno la mafundisho, mwingine ufunuo kutoka kwa Mungu, mwingine ataongea lugha mpya na mwingine atatafsiri hiyo lugha. Mambo yote yatendeke kwa ajili ya kujenga kanisa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi tuseme nini ndugu zangu? Mnapokutana pamoja, kila mmoja ana wimbo, au neno la mafundisho, au ufunuo, lugha mpya au atatafsiri. Mambo yote yatendeke kwa ajili ya kulijenga kundi la waumini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, ndugu, imekuwaje? Mkutanapo pamoja, kila mmoja ana zaburi, ana fundisho, ana ufunuo, ana lugha, ana tafsiri. Mambo yote na yatendeke kwa kusudi la kujenga.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndugu, tuseme nini, basi? Mnapokutana pamoja, mmoja aimbe wimbo, mwingine atoe mafundisho, mwingine awe na ufunuo kutoka kwa Mungu, mwingine atumie kipaji cha kusema kwa lugha ngeni na mwingine afafanue yanayosemwa. Yote yawe kwa ajili ya kulijenga kanisa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndugu, yafaayo ndiyo nini? Mnapokusanyika, kila mtu kama yuko na wimbo au fundisho au ufunuo au misemo migeni au mafumbuo yao, yote pia sharti yaje kujenga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, ndugu, imekuwaje? Mkutanapo pamoja, kila mmoja ana zaburi, ana fundisho, ana ufunuo, ana lugha, ana tafsiri. Mambo yote na yatendeke kwa kusudi la kujenga.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wandugu zangu, niseme nini basi? Wakati munapokusanyika kwa ibada, mumoja anaweza kuimba wimbo, mwingine kufundisha, mwingine kutoa ufunuo, mwingine kusema kwa luga za ajabu na mwingine anaweza kutafsiri. Na hayo yote yanapaswa kufanyika katika nia ya kujenga kanisa katika imani.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Imekuwaje bassi, ndugu? Mkutanapo pamoja, killa mmoja ana zaburi, ana fundisho, ana lugha, ana ufunuo, ana tafsiri. Mambo yote na yatendeke kwa kusudi la kujenga.