1 Corinthians 14:35 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ikiwa wanayo maswali ya kuuliza, wawaulize waume zao nyumbani, maana ni aibu kwa mwanamke kusema katika mikutano ya waumini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakitaka kuuliza kuhusu jambo lolote, wawaulize waume zao nyumbani. Kwa maana ni aibu kwa mwanamke kuzungumza katika kundi la waumini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao wakitaka kujifunza neno lo lote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wakiwa na jambo wanalotaka kujua, wawaulize waume zao nyumbani. Ni aibu kwa mwanamke kuzungumza pasipo utaratibu katika mikutano ya kanisa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ikiwa wanayo maswali ya kuuliza, wawaulize waume zao nyumbani, maana ni aibu kwa mwanamke kusema katika mikutano ya waumini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ikiwa wanayo maswali ya kuuliza, wawaulize waume zao nyumbani, maana ni aibu kwa mwanamke kusema katika mikutano ya waumini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama wakitaka kuuliza kuhusu jambo lo lote, wawaulize waume zao nyumbani. Kwa maana ni aibu kwa mwanamke kuzungumza kanisani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama wakitaka kuuliza kuhusu jambo lolote, wawaulize waume zao nyumbani. Kwa maana ni aibu kwa mwanamke kuzungumza kanisani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao wakitaka kujifunza neno lolote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ikiwa wanayo maswali ya kuuliza, wawaulize waume zao nyumbani, maana ni aibu kwa mwanamke kusema katika mikutano ya waumini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini wanapotaka kujifunza neno, na wawaulize waume wao nyumbani! Kwani haifai kabisa, mwanamke akisema penye wateule.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao wakitaka kujifunza neno lo lote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama wakiwa na neno la kuuliza, waulize waume wao kwenye nyumba zao. Ni haya kwa mwanamuke kusema katika mukutano wa kanisa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na wakitaka kujifunza neno, na waulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu, wanawake kunena katika kanisa.