1 Corinthians 14:6 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo, ndugu zangu, kama nikija kwenu na kusema nanyi kwa lugha ngeni itawafaa nini? Haitawafaa chochote, isipokuwa tu kama nitawaelezeni ufunuo wa Mungu au ujuzi fulani au ujumbe wa Mungu au mafundisho fulani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sasa ndugu zangu, nikija kwenu nikasema kwa lugha mpya, nitawafaidia nini kama sikuwaletea ufunuo au neno la maarifa au unabii au mafundisho?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ila sasa, ndugu, nikija kwenu na kunena kwa lugha, nitawafaidia nini, isipokuwa nasema nanyi kwa njia ya ufunuo, au kwa njia ya elimu, au kwa njia ya hotuba, au kwa njia ya fundisho?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndugu zangu, je, itawasaidia nikija kwenu na kusema kwa lugha zingine? Hapana, itawasaidia pale tu nitakapowaletea ufunuo mpya au maarifa fulani, unabii au mafundisho.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hivyo, ndugu zangu, kama nikija kwenu na kusema nanyi kwa lugha ngeni itawafaa nini? Haitawafaa chochote, isipokuwa tu kama nitawaelezeni ufunuo wa Mungu au ujuzi fulani au ujumbe wa Mungu au mafundisho fulani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo, ndugu zangu, kama nikija kwenu na kusema nanyi kwa lugha ngeni itawafaa nini? Haitawafaa chochote, isipokuwa tu kama nitawaelezeni ufunuo wa Mungu au ujuzi fulani au ujumbe wa Mungu au mafundisho fulani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sasa ndugu zangu, kama nikija kwenu nikasema kwa lugha mpya nitawafaidia nini kama sikuwaletea ufunuo au neno la maarifa au unabii au mafundisho?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sasa ndugu zangu, kama nikija kwenu nikasema kwa lugha mpya nitawafaidia nini kama sikuwaletea ufunuo au neno la maarifa au unabii au mafundisho?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ila sasa, ndugu, nikija kwenu na kunena kwa lugha, nitawafaidia nini, isipokuwa nasema nanyi kwa njia ya ufunuo, au kwa njia ya elimu, au kwa njia ya hotuba, au kwa njia ya fundisho?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo, ndugu zangu, kama nikija kwenu na kusema nanyi kwa lugha ngeni itawafaa nini? Haitawafaa chochote, isipokuwa tu kama nitawaelezeni ufunuo wa Mungu au ujuzi fulani au ujumbe wa Mungu au mafundisho fulani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini sasa, ndugu, kama ningekuja kwenu na kusema misemo migeni, ningewafaa nini, nisiposema nanyi nikiifunua au nikiitambulisha au nikiifumbua au nikiifundisha?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ila sasa, ndugu, nikija kwenu na kunena kwa lugha, nitawafaidia nini, isipokuwa nasema nanyi kwa njia ya ufunuo, au kwa njia ya elimu, au kwa njia ya hotuba, au kwa njia ya fundisho?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi wandugu zangu, nitawafalia nini kama nikikuja kwenu na kusema nanyi katika luga za ajabu? Sitawafalia kitu pasipo kuwaelezea maneno ya ufunuo, au ya elimu, pasipo kuwatabiria au kuwafundisha.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi, ndugu, nikija kwenu na kunena kwa lugha, nitawafaidia nini, isipokuwa nanena nanyi kwa njia ya ufunuo, au kwa njia ya elimu, au kwa njia ya khotuba, au kwa njia ya fundisho?