1 Corinthians 14:9 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hali kadhalika na nyinyi, kama ulimi wenu hausemi kitu chenye kueleweka, nani ataweza kufahamu mnayosema? Maneno yenu yatapotea hewani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Vivyo hivyo na ninyi, mkinena maneno yasiyoeleweka katika akili, mtu atajuaje mnalosema? Kwa maana mtakuwa mnasema hewani tu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Vivyo hivyo na ninyi, msipotoa kwa ulimi neno lililo dhahiri, neno lile linenwalo litajulikanaje? Maana mtakuwa mkinena hewani tu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndivyo ilivyo hata kwenu ninyi. Watu hawataweza kuelewa unachosema, ikiwa utazungumza katika lugha tofauti wasiyoitambua. Utakuwa unazungumza hewani tu!
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hali kadhalika na ninyi, kama ulimi wenu hausemi kitu chenye kueleweka, nani ataweza kufahamu mnayosema? Maneno yenu yatapotea hewani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hali kadhalika na nyinyi, kama ulimi wenu hausemi kitu chenye kueleweka, nani ataweza kufahamu mnayosema? Maneno yenu yatapotea hewani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Vivyo hivyo na ninyi, kama mkinena maneno yasiyoeleweka katika akili, mtu atajuaje mnalosema? Kwa maana mtakuwa mnasema hewani tu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Vivyo hivyo na ninyi, kama mkinena maneno yasiyoeleweka katika akili, mtu atajuaje mnalosema? Kwa maana mtakuwa mnasema hewani tu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Vivyo hivyo na ninyi, msipotoa kwa ulimi neno lililo dhahiri, neno lile linenwalo litajulikanaje? Maana mtakuwa mkinena hewani tu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hali kadhalika na nyinyi, kama ulimi wenu hausemi kitu chenye kueleweka, nani ataweza kufahamu mnayosema? Maneno yenu yatapotea hewani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Vivyo hivyo nanyi mnaposema misemo migeni isiyojulikana, yale maneno yenu yatatambulikanaje? Kwani mtakuwa kama wanaojisemea tu na kupigia upepo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Vivyo hivyo na ninyi, msipotoa kwa ulimi neno lililo dhahiri, neno lile linenwalo litajulikanaje? Maana mtakuwa mkinena hewani tu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ni hivi vilevile mambo munayosema yatatambulikana namna gani ikiwa maneno munayoeleza kwa luga za ajabu hayako wazi? Kwa maana mutakuwa kama wenye kusema na upepo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Vivyo hivyo na ninyi, msipotoa kwa ile lugha neno lililo dhahiri, neno lile linenwalo litajulikanaje? Maana nitakuwa mkinena katika hewa tu.