1 Corinthians 15:12 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sasa, maadamu inahubiriwa kwamba Kristo amefufuliwa kutoka kwa wafu, baadhi yenu wanawezaje kusema kwamba hakuna ufufuo wa wafu?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi kama tumehubiri kwamba Al-Masihi alifufuliwa kutoka kwa wafu, mbona baadhi yenu mnasema hakuna ufufuo wa wafu?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, ikiwa Kristo anahubiriwa ya kwamba amefufuka katika wafu, mbona baadhi yenu husema kwamba hakuna kiyama ya wafu?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tunamwambia kila mtu kuwa Kristo alifufuliwa kutoka kwa wafu. Hivyo kwa nini baadhi yenu mnasema watu hawatafufuliwa kutoka kwa wafu?
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Sasa, maadam inahubiriwa kwamba Kristo amefufuliwa kutoka wafu, baadhi yenu wanawezaje kusema kwamba hakuna ufufuo wa wafu?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sasa, maadamu inahubiriwa kwamba Kristo amefufuliwa kutoka kwa wafu, baadhi yenu wanawezaje kusema kwamba hakuna ufufuo wa wafu?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi kama tumehubiri ya kwamba Kristo alifufuka kutoka kwa wafu, mbona baadhi yenu mnasema hakuna ufufuo wa wafu?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi kama tumehubiri ya kwamba Al-Masihi alifufuliwa kutoka kwa wafu, mbona baadhi yenu mnasema hakuna ufufuo wa wafu?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, ikiwa Kristo anahubiriwa ya kwamba amefufuka katika wafu, mbona baadhi yenu husema kwamba hakuna kiyama ya wafu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sasa, maadamu inahubiriwa kwamba Kristo amefufuliwa kutoka kwa wafu, baadhi yenu wanawezaje kusema kwamba hakuna ufufuo wa wafu?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Lakini Kristo akitangazwa, ya kuwa amefufuka katika wafu, kwenu wengine husemaje: Hakuna ufufuko wa wafu?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, ikiwa Kristo anahubiriwa ya kwamba amefufuka katika wafu, mbona baadhi yenu husema kwamba hakuna kiyama ya wafu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ikiwa tunahubiri kuwa Kristo amefufuka, namna gani basi wengine kati yenu wanasema kama wafu hawatafufuka?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi, ikiwa Kristo amekhubiriwa kwenu ya kwamba amefufuka, mbona wengine wenu wasema kwamba hakuna kiyama ya wafu?