1 Corinthians 15:24 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya hayo, mwisho utafika wakati ambapo Kristo atamkabidhi Mungu Baba ufalme, baada ya kufutilia mbali kila tawala na mamlaka na nguvu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo mwisho utafika, atakapomkabidhi Mungu Baba Mwenyezi ufalme, baada ya kuangamiza kila utawala na kila mamlaka na nguvu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndipo mwisho utakuja. Kristo atamwangamiza kila mtawala na kila mamlaka na nguvu. Kisha atampa Mungu Baba ufalme.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Baada ya hayo, mwisho utafika wakati ambapo Kristo atamkabidhi Mungu Baba Utawala, baada ya kufutilia mbali kila tawala na mamlaka na nguvu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya hayo, mwisho utafika wakati ambapo Kristo atamkabidhi Mungu Baba ufalme, baada ya kufutilia mbali kila tawala na mamlaka na nguvu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo mwisho utafika, wakati atakapomkabidhi Mungu Baba Ufalme, akiisha angamiza kila utawala na kila mamlaka na nguvu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo mwisho utafika, wakati atakapomkabidhi Mungu Baba ufalme, akiisha angamiza kila utawala na kila mamlaka na nguvu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya hayo, mwisho utafika wakati ambapo Kristo atamkabidhi Mungu Baba ufalme, baada ya kufutilia mbali kila tawala na mamlaka na nguvu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
mwisho ni hapo, atakapompa Mungu Baba ufalme, ni hapo, atakapokuwa amekwisha kuutangua ukubwa wote na nguvu na uwezo wote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na nyuma ya pale, mwisho wa vyote utatimia. Wakati ule Kristo ataharibu utawala wote, mamlaka yote na uwezo wote, naye atamupatia Mungu Baba ufalme.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ndipo palipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu.