1 Corinthians 15:27 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana, Maandiko yasema: “Mungu ameweka vitu vyote chini ya miguu yake.” Lakini, Maandiko yanaposema: “Vitu vyote vimewekwa chini ya miguu yake avitawale” ni dhahiri kwamba Mungu haingii katika kundi hilo la vitu, maana yeye ndiye anayeviweka vitu hivyo chini ya Kristo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana Mungu “ameweka vitu vyote chini ya miguu yake”. Lakini isemapo kwamba “vitu vyote” vimewekwa chini yake, ni wazi kwamba Mungu aliyetiisha vitu vyote chini ya Al-Masihi hayumo miongoni mwa hivyo vilivyotiishwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa, Alivitiisha vitu vyote chini ya miguu yake. Lakini atakaposema, Vyote vimetiishwa, ni dhahiri ya kuwa yeye aliyemtiishia vitu vyote hayumo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kama Maandiko yanavyosema, “Mungu ameweka kila kitu chini ya udhibiti wake.” Inaposema “kila kitu” kimewekwa chini yake, hii ni wazi Mungu peke yake ndiye ambaye hayuko chini yake. Mungu ndiye anayeweka kila kitu chini ya udhibiti wa Kristo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana, Maandiko yasema: “Mungu ameweka vitu vyote chini ya miguu yake.” Lakini, Maandiko yanaposema: “Vitu vyote vimewekwa chini ya miguu yake avitawale” ni dhahiri kwamba Mungu haingii katika kundi hilo la vitu, maana yeye ndiye anayeviweka vitu hivyo chini ya Kristo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana, Maandiko yasema: “Mungu ameweka vitu vyote chini ya miguu yake.” Lakini, Maandiko yanaposema: “Vitu vyote vimewekwa chini ya miguu yake avitawale” ni dhahiri kwamba Mungu haingii katika kundi hilo la vitu, maana yeye ndiye anayeviweka vitu hivyo chini ya Kristo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana Mungu “ameweka vitu vyote chini ya miguu yake.” Lakini isemapo kwamba “vitu vyote” vimewekwa chini yake, ni wazi kwamba Mungu aliyetiisha vitu vyote chini ya Kristo hayumo miongoni mwa hivyo vilivyotiishwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana Mungu “ameweka vitu vyote chini ya miguu yake.” Lakini isemapo kwamba “vitu vyote” vimewekwa chini yake, ni wazi kwamba Mungu aliyetiisha vitu vyote chini ya Al-Masihi hayumo miongoni mwa hivyo vilivyotiishwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa, Alivitiisha vitu vyote chini ya miguu yake. Lakini atakaposema, Vyote vimetiishwa, ni dhahiri ya kuwa yeye aliyemtiishia vitu vyote hayumo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana, Maandiko yasema: “Mungu ameweka vitu vyote chini ya miguu yake.” Lakini, Maandiko yanaposema: “Vitu vyote vimewekwa chini ya miguu yake avitawale” ni dhahiri kwamba Mungu haingii katika kundi hilo la vitu, maana yeye ndiye anayeviweka vitu hivyo chini ya Kristo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani aliyaweka yote chini miguuni pake. Lakini pakisemwa: Yote yaliwekwa chini yake, iko waziwazi, ya kuwa ndiyo yote pasipo yule aliyeyaweka yote chini yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuwa, Alivitiisha vitu vyote chini ya miguu yake. Lakini atakaposema, Vyote vimetiishwa, ni dhahiri ya kuwa yeye aliyemtiishia vitu vyote hayumo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana Maandiko Matakatifu yanasema: “Mungu aliweka vitu vyote chini ya miguu yake.” Ndiyo Maandiko Matakatifu yanasema kwamba alipewa mamlaka juu ya vitu vyote. Lakini maneno haya yanaonyesha wazi kwamba Mungu hahesabiwi katika hili neno “Vyote”, kwa maana ni yeye aliyemupa mamlaka juu ya vitu vyote.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa kuwa alitiisha vitu vyote chini ya miguu yake. Lakini akisema, Vyote vimetiishwa, ni dhahiri ya kuwa yeye aliyemtiishia vitu vyote hamo.